Kama DUNIANI kila mtu angekuwa PROFESA!
>> Monday, May 09, 2011
DUNIANI,...
....ingawa inasemekana kuna mpaka WATEMBEAO KAMA BATA kwenye mwendo wao wa MARINGO,...
SWALI:
- Hivi kwani ukitafiti si labda kila MTU kuna kitu anajua zaidi?
- Na hivi ni kweli PROFESA wa KITU ndiye mjuaji zaidi KITU?
Na katika DUNIA ambayo kila mtu ni PROFESA wa kitu fulani,....
- Si BINADAMU bado wangetafuta jinsi ya kuona wengine ni MAPROFESA zaidi?
Na DUNIANI kama kila mtu angekuwa MJINGA,...
.... labda WAJINGA wangemteua profesa wao wa UJINGA!:-(
Nawaza tu MKUU!
Jumatatu njema MHESHIMIWA!
Hebu Sam Mangwana arudishe pini- Mokolo Nakokufa / Minha Angola
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nilikuwa sijui Profesa hasa ni mtu gani mpaka sasa hivi nilipofanya pekua pekua na kamusi ya Kizungu. Kumbe si lazima awe na Phd?
Nami nitaomba mwaka ujao nipigiwe kura kusudi niwe Prof.
Au kama sio kura, wanapatapataje wenzetu uprofesa huo, watupatie siri kidogo nasi!
@Mkuu Goodman: Nafikiri kuna MAPROFESA kadhaa mtandaoni ambao tuwasubiri watekenye jibu!
Hivi kwani si cheo tu prof. kama vile Dr, headmaster nk...ambapo inasemekana pia ni binadamu kama mimi na wewe na yeye? Hakika kila siku watu tunazidi kuelimishana humu kwenye hizi blog...mmmhh najiwazia tu kama ni kweli....
Ndio kuna uprofesa wa shule, tunaukubali,...wapo kweli sio mchezo, lakini hata akiwa profesa, sio lazima ajue kila kitu katika nyanja hiyo aliyoisomea..! Au nimekosea ?
mmm wala hujakosea kabisa mie naungana nawe...kwani katika ubinadamu lazima kuna kukosea...
Basi wasije wakafanya kosa lakunifanya mimi ndie raisi wakwanza duniani kotekote, la sivyo nitalazimisha asiitwe mtu yeyote yule "profesa" ila tu kama anayo shahada ya DOCTORATE kwisha!
Post a Comment