Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo katika Simon Kitururu kugombezwa na mwanadada: Koma kutumia neno JIKO wakati unaongelea MWANAMKE anayeolewa!:-(

>> Tuesday, May 03, 2011

Katika gumzuzo LEO sentensi zilienda....


Simon Kitururu:

-Ndio  mdau yule kapata jiko juzijuzi tu  na nasikia Jiko lake tayari mambo fulu kichefuchefu asubuhi - yani mambo tayari  kikuujaza ulimwengu baada ya miezi kadhaa!

Mdada (Jina kapuni):
-Simon sikuwahi kustukia kuwa wewe sexist namna hiyo. Kumbe na wewe  wake za watu unawaona ni JIKO.  Kwa mfano mie sipiki hata siku moja kwangu  mambo ya jiko ni ya Mume wangu hayo kwanza anajua zaidi kupika na pia mie ndio nashinda kazini muda mrefu na  mwenye mshahara Mkubwa . Sasa nani hapo JIKO?

Simon Kitururu katika kujitetea:

Ebwana sikumaanisha hiyo kitu kihivyo Mrembo! Nafikiri unajua kuna maneno tu  saa nyingine hutumika na nahisi unajua nilikuwa simaanishi yani mwanamke kazi yake ni jikoni au tu kumpikia mumewe bila kusahau .....

Kabla sijaendelea Mdada akanikata: Kwanza MREMBO nani! SI unaona  hata tunavyoongea unaanza kuniita MREMBO sijui nini ili kisaikolojia kuniweka matawi ya chini  kuwa ponti zangu kwa kuwa na sura nzuri ni za kijinga!Halafu huu mfumo dume wenu huu unafanya nyie midume mnyanyase wanawake kirahisi tu kwa kuwa Jamii inaona sawa tu hata kauli zenu mtumiazo hata kistaarabu ambazo ni passive aggressive towards women.........


Anewei.....
.... nilirudi matawi ya chini na kuwa muangalifu katika misamiati nayo tumia  mpaka mazungumzo  na MDADA yalipobadilika na stori za Rais Obama kafeki kifo cha Osama Bin Laden yalipoingilia kati  nyambisi!:

Swali:
  • Ushastukia kuna wadada wanachukia wakisikia sentensi``Fulani kapata JIKO ´´ kwa kuwa wanaona MWANAMKE anadhalilishwa?

Eniwei,..
.-.. nimestukia hilo leo,...
... ndio kila siku kuna jipya mtu unaweza kujifunza.

AU?

Hebu Ray Charles anisaidie kubadili wazo kwa  - The Sun Died


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 12:33 pm  

Mkuu kweli ulimi...ulimi unatakiwa kuchungwa!

Yasinta Ngonyani 1:52 pm  

Haswa ...ulimi hauna mfupa...

Mwanasosholojia 4:23 pm  

Mimi sidhani kama ni tatizo kutumia neno JIKO kwa mwanamke aliyeolewa. neno JIKO linatumika symbolically kutokana na umuhimu wake positively. JIKO ni muhimu sana ndani ya nyumba au familia, bila jiko sidhani kama mnaweza kuandaa chakula chenu wenyewe ndani. Kwa kawaida lazima mtu uingie jikoni (hata kama haimaanishi hapa kuwa wanaume wengi hawapiki na wanaopika ni wnawake tu). Mimi nafikiri dada yetu yeye alitafsiri "kavu kavu" bila kuruhusu kufikiria neno JIKO lina mantiki gani na kwa nini litumike kwa mwanamke aliyeolewa. Mimi sioni tatizo hapo na ninachoona ni heshima kubwa anayopewa mwanamke aliyeolewa, wala si mambo ya sexism.

Simon Kitururu 4:31 pm  

@Mwanasosholojia: Na mimi mtazamo wangu ulikuwa kama wako kabla ya kugongana na Mdada ambaye anahisi vingine! Ila unajua tena siku hizi katika mambo ya usawa kati ya mwanamke na mwanaume upiganiwao sana na MAFEMINIST zaidi -unaweza kujikuta maneno uliyozoea yanaangaliwa kwa jicho tofauti kwa nia ya kuhakikisha BINADAMu wote ni sawa.

Siku hizi hata kwa KIINGEREZA kuna maneno kibao ambayo ukitumia kwa ma- FEMINIST au hata wasenge ,... utaonekana hauko Politically Correct.

Halafu nafikiri neno JIko katika matumizi yangu leo liliniingia akilini na kuanza kulitumia baada ya kupita kwenye Blogu yako ambako umelitumia.

Kwa hiyo kimtazamo mwingine wa kinamna :

Ni wewe uliyeniponza Mwanasosholojia!:-)

Mwanasosholojia 5:21 pm  

Ni kweli kabisa Mtakatifu, teh! pole sana, ni mtazamo tu kama unavyosema,hatuko sawa. Katika dunia hii kukumbana na hali kama hizi hasa kwa sisi mabloga ni kitu cha kawaida..unafanya kama ulivyofanya,unatumia nafasi ku-clarify..ukiona bado hakieleweki basi una-apologize na kucheck usawa mwingine. Gender issues bwana ni social construction!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP