Na ni kweli LABDA hakuna AHITAJIYE kiongozi katika safari ya kwenda CHOONI!
>> Tuesday, May 31, 2011
SwaLi:
- Kwani unafikiri SAFARI ya viongozi wetu AFRIKA ni yakuelekea CHOONI au SEBULENI kwenye ubwabwa?
Katika AFRIKA ambayo imejaa VIONGOZI watakao tu kuitwa VIONGOZI ,...
.... huku tukijiuliza kuwa pamoja na NIA na MADHUMUNI yao ni kuitwa VIONGOZI labda huwa hawajafikiria kuwa KUONGOZA ambako kunaambatana na jina ``KIONGOZI´´ ni NINI,...... labda WAONGOZWAO inabidi kukumbuka tu kuwa kuna MENGI wala hayahitaji KIONGOZI ili yafanikiwe,....
.... hasa ukizingatia labda waitwao VIONGOZI kuongoza sio moja ya TALANTA waliojaliwa na MWENYEZI .:-(Swali:
- Kwani unauhakika VIONGOZI wako wanajua wanapeleka wapi WANANCHI au wanabunia?
- SI inasemekana kuna wenye nia na MADHUMUNI ya kuwa tu VIONGOZI ingawa kuongoza ni kitu wastukiacho baadaye kuwa kinahitaji MTU ajue KUONGOZA na jina KIONGOZI tu halitoshi?
Ndio,...
.... labda WANANCHi inabidi wajiongoze tu katika mengi wao wenyewe,...
.... kwa kuwa ni MENGI tu labda hayahitaji waongozwe hata kama HAPA hatuongelei maswala ya safari za kuelekea CHOONI hasa kama ahusikaye sio MTOTO!:-(Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu Banana Zorro arudie-Mama Yangu
Maunda Zorro arudie -Nafurahi
Zahir Ally Zorro Feat Mr Blu na Baby Boy warudie-Fanya Vitu Vyako
7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Simon! "kweli hakuna anayehita kiongozi katika safari ya kwenda chooni?"Ahsante kwa wimbo wa Maunda zorro nimeupenda sana:-)
Familia ya Zorro Hiyo!
Kiongozi mwema ni yule anayejua kuwa anaowaongoza `ndio waliomuajiri' katika siasa,kwasababu, kama hawapo utamuongoza nani!
Lakini kweli ukizaliwa tu wewe mwenye ni kiongozi, hilo ni la muhimu, ila ili jamii iwe na msemaji mkuu, msimamizi wa hili na lile! Inawajibika kuwa na mteule fulani, swali kubwa ni nani?
@Yasinta: NI kweli! Ila ,....
@M3: Ukifuatilia SERIKALI kibao ambazo hujua wafanyacho KIONGOZI huwa na MSEMAJI WAKE aka Spokesperson.
Na na labda kama kila mtu angekuwa anafanya kile atakiwacho kufanya USIMAMIWAJI hauhitajiki sana kwa BINADAMU ambaye ni mwenyewe kajitungia maswala ya UONGOZI na mifumo ya UONGOZI yafanyayo mpaka sasa DUNIANI tunahangaika na swala la tufuate DEMOKRASIA au kitabu kitukufu kishauricho SHARIA ndio JIBU .
DUH umeniwazisha upya swala MKUU !
VIPI Simon mbona umesema "Ni kweli ila....Je nimekosea?
Hii fikra ya leo!!
kaka umenena umefanya siku yangu iwe ya kutafakari juu ya hili.Tena wengine hawajui hata tafsiri ya uongozi ni nini...SASA KUNA UMUHIMU GANI WAKUWA NA KIONGOZI?
Siku inakaribia hapo sifa za uongozi si ukoo wako wala utajiri wala elimu....
... bali KASHFA TUPU!!!
Kwa kuwa hakuna familia isiekuwa na kashfa, mimi ningemchagua kiongozi mtu atakaeniambia:
"Baba alikuwa mvuta bangi; mama aliwahi kuingia jela kwa mawuaji; mtoto wangu wa kwanza ni malaya wa kiume; mimi mwenyewe nilisoma shule huko Ulaya huku nikiwa nauza madawa ya kulevya..." na kadhalika.
Kifupi, Bwana Kitururu, Mkuu: Tumechoka sana na kupata viongozi waliopambwapambwa! Sasa tunataka viongozi wanaofanana nasi NA HAPO WATUAMBIE JINSI WALIVYOIBUKA DHIDHI YA UGUMU NA KASHFA ZOTE ZA KIFAMILIA NA KIJAMII ZAO.
Post a Comment