Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo katika KISWANGLISH: Don't JUDGE a book/KITABU by chupi yake!

>> Sunday, May 08, 2011

JALADA nishai,...
... hasa kwa kuwa hata kitabu cha KEMIA kinaweza kujaladiwa kwa  gazeti la sauti ya INJILI la KKKT  au lile tu  la UDAKU  wa hivi ni kweli  kwa kuwa MHESHIMIWA  kaonekana anakula kwa MAMA NTILIE kwa hiyo kashachachishwa na nyumba ndogo!:-(

NA labda it is bomba  la UKWELI kuwa ,...
.... kwa papara papara unaweza JUDGE  na kupata CHUPI SAFI  kwa nje,....
..... wakati kwa ndani kuna ushahidi wa mpaka wa ramani za mikojo kuwa KIFICHA NYETI hicho  kichafu aisee!:-(



Swali:

  • Kwani si inasemekana ni URAHISI tu wa  watu KURAHISISHA mambo ndio usababishao WATU wahitimishe  kitu  kwa kukiangalia tu kwa JUU JUU?

  • Na si  inawezekana  ni maamuzi kibao labda hata wewe umefikia kwa kuwa tu KWA JUU sio matusi na   SAMAKI kwa nje haonekani kaoza na anamafinyofinyo kwa ndani?

Ndio,...
... labda tuliza MANYANGA na tafakari undani hata wa KISURA,....
... kabla ya kuhitimisha kuwa  mnono ni MNONO  kwa kuwa kwa nje KANONA.:-(

Ni wazo tu hili BINGWA na usikonde NGULI!:-(




Au tu Peter Tosh arudie - The Toughest

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:59 am  

Nukuu "Swali:


Kwani si inasemekana ni URAHISI tu wa watu KURAHISISHA mambo ndio usababishao WATU wahitimishe kitu kwa kukiangalia tu kwa JUU JUU?


Na si inawezekana ni maamuzi kibao labda hata wewe umefikia kwa kuwa tu KWA JUU sio matusi na SAMAKI aonekani kaoza na anamafinyofinyo kwa ndani?" mwisho wa nukuu....Hii nimeipenda sana kwani ni mara nyingi sana watu wengi wanafanya hivi na huwa inaniuma SANA. Ahsante kwa kuandika hili.

Simon Kitururu 9:00 am  

@Yasinta:Asante kwa kupenda mtiririko wa wazo mtu wangu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP