Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda hakuna MWANASIASA afanyaye kazi za KISIASA asiye MUONGO !:-(

>> Thursday, May 05, 2011

Ndio,...
.... MOJA ya sifa  na kifaa cha kufanikishia SIASA,...
... kwa MWANASIASA ni uwezo wake wa KUDANGANYA!:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Au unataka kusema hustukii akina Waziri Mkuu NYERERE, Obama, Museveni, au tu Mwenyekiti wa  KITONGOJI  akiwa kazini moja ya silaha yake ya kazi ni nini?

Na haki ya nani ,...
.... hata kama HUAMINI,.....
... ila kama UMEWAHI  KUSIKILIZA MWANASIASA akiongea tu  na tuachilie mbali AKIHUTUBIA,...
.... basi wewe labda jua tu kuwa UMESHAWAHI  kudanganywa wewe!:-(



Swali:
  • Unabisha?

Na MWANASIASA mzuri ni yule mwenye staili ya kudanganya ambayo  hata akidakwa,...

.. anaweza kuja na visababu kedekede vya ni kwanini hakusema kweli !:-(

Swali:
  • SI umeshawahi kusikia MWANASIASA akidai kuwa KWA SABABU ZA KIUSALAMA wa TAIFA bla blabla blabla ilibidi ``KWELI´´ asiiseme hadharani?

Ndio,...
.... kuna wakudanganyao hasa wakati wanatumia hata sentensi zianzazo na  maneno kama:
``Kusema UKWELI.....´´
``Ukweli ni kwamba...´´

.... kama tu wadau wakudanganyao watumiavyo  maneno kama :
``SIKUDANGANYI '' katika sentensi kama:
  `` Haki ya nani sikudanganyi  Bi NYONYO kapigwa mtungo na wanafunzi wake - wakati inajulikana Bi NYONYO  ni dume jike na ndiye haswa apigaye mtungo  watoto wa watu kwenye SHULE ya SEKONDARI ya WASICHANA afundishayo  hasa kwa kuwa WATU  wanafikiri Miss NYONYO ni Mwalimu wa KIKE kwa kuwa  ana NYONYO´´ ...

..AU sentensi zenye maneno :
``KWELI KABISA.... ´´ kama katika sentensi kama 
`` Kweli kabisa  nilishuhudia  kwa macho yangu Bin Laden anapata kikombe kwa Babu Loliondo - wakati mdau akusimuliaye unajua ni KIPOFU´´.:-(


Ni wazo tu hili Mheshimiwa!:-(
SIKU NJEMA !

Hebu tu tena St. Germain warudie tu tena mdinyo-Sure THING



St Germain watekenye tu tena -Rose Rouge



Au tu St. Germain watumbue tu kabisa kwa -SO FLUTE

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 3:27 pm  

Sawa mzee wa tungo.

Rachel Siwa 8:58 pm  

hahahahh!na miaka yao inaisha ahadi hazitimii,yaani uongo ndiyo Agano la Siasa!!!!
kwikwiwki Bi nyonyo,@kaka wa mimi unamaneno wewe.

Simon Kitururu 9:56 pm  

@Rasta Mcharia +Da Rachel: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP