Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kitu kizuri KWA MTU ikiwa ni kile USICHOKIPENDA!

>> Sunday, May 22, 2011

Kipendwacho ,....
....na KITU kizuri ,...
.... inaweza kuwa ni VITU viwili tofauti,...
.... ingawa wengi hufikiria kwa kuwa wanapenda KITU basi hicho ni kitu KIZURI!


Na kitu KIZURI kinaweza kuwa ni kile kichungu kama klorokwini,...
..... hata kama kwa kuwa ni kichungu,...
... basi HAKIPENDWI!:-(

Swali:
  • SI nyama ya nguruwe ni kitu kizuri kwa apendaye KITI moto ingawa labda MLENDA na MCHICHA   ndio kikweli ni kitu KIZURI?
  • Kwani unafikiri hata sasa hivi UPENDACHO  hakuna uwezekano kama unafikiria ni KIZURI labda ni kwa kuwa umependa tu na usingekuwa umependa labda ungeshastukia kuwa kinanuka zaidi ya  kikwapa?
Ndio,...
.... labda JITU ZEE ndio zuri,...
.... hata kwa apendaye DOGO DOGO   kwa kuwa tu KAPENDA,...
...na kwa hiyo DOGO DOGO kwake   limegeuka ni saizi yake na kwahiyo ZURI!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumapili NJEMA!


Hebu Jamiroquai wabadili wazo kwa -Virtual Insanity



Au sijui kwanini hebu tu Jason Baptise arudie tu tena- De Garden Want Water


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:01 am  

nukuu "Swali:

SI nyama ya nguruwe ni kitu kizuri kwa apendaye KITI moto ingawa labda MLENDA na MCHICHA ndio kikweli ni kitu KIZURI?
Kwani unafikiri hata sasa hivi UPENDACHO hakuna uwezekano kama unafikiria ni KIZURI labda ni kwa kuwa umependa tu na usingekuwa umependa labda ungeshastukia kuwa kinanuka zaidi ya kikwapa?" Nakubaliana nawe 100% kabisa:-)

Simon Kitururu 12:01 pm  

@Yasinta: :-)

Yasinta Ngonyani 12:07 pm  

Leo ni mara ya kwanza kuona mtakatifu Simon anaandika hii alama:-)....nami nasema Simon:-) Dominika njema mlongo wangu!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP