Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika KUJALI kwa waonekanao WAKATI kilema kaanguka HAWAJALI!

>> Thursday, May 19, 2011

Saa nyingine inabidi ujue MTU ili,...
.... ujue staili yake ya KUJALI,....
... kama tu saa nyingine ihitajikavyo ujue ni nani ni kweli ANAMLILIA MAREHEMU MSIBANI katika  vilio vya waliao MSIBANI ,...
.... hasa ukizingatia  inawezekana yule asiye dondosha chozi hata tone  MSIBANI ndiye anaweza kuwa anahuzuni kuliko yule mwenye  kulia kwa sauti kama FISI kabanwa na mfupa MSIBANI huku akibubujika CHOZI  kipimo PIPA.:-(

Swali:
  • Si ushastukia mara nyingine AKUJALIYE ni yule akuachiaye utatue MATATIZO yako pekee ili  ungangamare na akuharibuye KWA KUTOKUJALI  ni yule  kilaini  tu anakutafutia KIDUDE ili usisumbuke kustukia KIDUDE kinapatikanaje kitu ambacho  kinaweza kuathiri hata jinsi uthaminivyo KIDUDE kwa kuwa ushazoea ukitaka tu unaletewa wakati kilainishwa kabisa ili ule kilaini?

KUJALI KWA MTU  inawezekana moja ya siri yake ,....
.... ni hutobolewa na MTU pale anapojifanya HAJALI,....
.... na kwa mtu KUJIFANYA hajali WATU wanasema nini kuhusu YEYE kiudaku ,....
..... inaweza kuwa ndio anatoboa siri kuwa pamoja na kuamini uzuri wa mtu ni TABIA,...
..... lakini   tetesi kuwa KALIO lake KIMTUNO  ni kwa msaada wa madawa ya MCHINA ni kitu kinacho mkunisha kichwa pia kwa kuwa  haki yanani angesifiwa  kalio pia kwa kuwa anajijua anaTABIA nzuri,....
..... angeua ndege wawili katika KUJISIKIA vizuri kwa hiyo ANAJALI.:-(

Swali:
  • Kwani unadhani Simon Kitururu hajali ya HEKIMA na BUSARA wakati anaandika UJINGA?
  • Si unajua kunawajifanyao HAWAJALI hadharani tu?



Ndio,...
.... labda kila MTU anastaili zake za KUJALI vitu,...
.... na kunaunaofikiri HAWAKUJALI kwa kuwa kuna vitu unategemea kama WANAKUJALI wangefanya,...
... lakini MAISHANI  wengine ungejua yanayowasibu  na wajisikiavyo wakokibanoni ,...
... labda ungestukia kuwa moja ya wanavyojaribu tu kukabiliana  na kuendelea na siku ,....
... ndicho kisababishao wengine wapigao chabo kwa pembeni kuona JAMAA hajali na anampita hivihivi KILEMA  aliyeanguka!:-(


Swali:
  • Kwani unafikiri UJALIVYO kila mtu anastukia UNAJALI?

Ndio,....
..... labda kunawanaokujali udhaniao HAWAKUJALI  kwa vitendo vyao hivyo hivyo vya kukunyima,...
... na wale udhaniao wanakujali kwa kuwa wanakugaia ,....
... wakati wanakugaia yoteyote  KIGAWIO chao kimejaa  Kaswende, Gono , Mdudu na Uharisho kidoooogo,...
....kwa kuwa  ukarimu wao kivitendo unamisingi katika ukweli HAWAKUJALI !:-(


Ni wazo tu hili MKUU!:-(

Au hebu tutulize WAZO  kwa......



Au kwa....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP