Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika JUHUDI ZA WENGI wanadamu wanamchezo wa KUWASIFIA wachache!

>> Tuesday, May 10, 2011

Na kwa kuwa katika ya WENGI ,...

... ni wachache JUHUDI zao WANADAMU huwa na MCHEZO wakuzikumbuka,....
..... kwahiyo KUMBUKA,...


.... wakati Rais NELSON MANDELA au hata Rais NYERERE anasifiwa kwa aliyofanya,.....
.... kuna WENGI walihusika katika YAWASIFIWAO  na KIBINADAMU hawakumbukwi tu!:-(

Swali:
  •  Unabisha?
  • Unafikiri PELE kwenye kabumbu angekuwa mkali hivyo kama hakuna wengine kwenye KABUMBU waliochangia?
  • Unafikiri  ya hekima za  BUDDHA mpaka yanakufikia ni mchango wa BUDDHA pekee na wengine hawajahusika?

Ndio,....
... labda ukisikia MTU anasifiwa,...
... kumbuka kitendo hicho labda ndio kifunikacho wengine wastahilio KUSIFIWA!:-(

Ni wazo tu hili BINGWA!:-(

Au tu hebu  Mos DEF, Ben Jaffe, Lenny Kravitz, Trombone Shorty, Tim Robbins na The Preservation Hall JAZZ  BAND wa Jam



Au tu na  Msondo Ngoma Music Band watulize manyanga kwa- Mama


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 6:01 pm  

Mimi nakuonea wivu sana, Simon; labda hata kukuchukia pia.


Nilikuwa nawaza asubuhi kwenye blogu yangu niingize mambo ya mmoja katika hao wazee uliewataja, na nikasita... KUMBE WEWE HUSITI KAMWE!


Naam! Leo ni barabara (YAANI, EXACTLY, KABISA) miaka 17 tangu raisi wa kwanza mswahili kuingia madarakani Afrika Kusini- INAUGURATION http://en.wikipedia.org/wiki/Nelson_Mandela


Katika mawazo ya wengi, viongozi hawa wanaonekana leo kama Mungu kabisa, na hapo umenena!


Hiyo nikutokana na kwamba vyombo vya habari vilimilikiwa na watu kadha wa kadhaa wenyewe wakiwa ni wenye fikra za kikoloni... yaani MONOPOLY OF THE MASS MEDIA BY THOSE WHO HAD A COLONIAL AX TO GRIND.

Leo Simon Kitururu akiwa Raisi wa kwanza Jamhuri wa Muungano Wa Afrika hatutamtukuza kama Mungu kutokana na hali halisi: WANABLOG WANABLOGI KILA SIKU KUHUSU MCHANGO WA KILA KIUMBE CHA MUNGU KINACHOCHANGIA HADI HALI HIYO YA UNITED STATES OF AFRICA!

malkiory 6:34 pm  
This comment has been removed by the author.
Malkiory Matiya 6:36 pm  

Kitururu Nyerere na mandela watabakia kuwa viongozi wasiosahulika katika ulingo wa siasa kwa kutokuwa wabinafsi. Kilichochangia wachukuliwe kama miungu wadogo ni elimu ndogo miongoni mwa watu waliokuwa wakiwaongoza.

Simon Kitururu 8:31 am  

@Mkuu Goodman: Unajua moja ya chanzo cha taralila hii ni nilikuwa namsikiliza Mugabe akimuongelea Bishop Tutu na ufinyu wa mchango wake kwenye ukombozi wa Afrika Kusini ukilinganishwa na asifiwavyao hasa Ughaibuni!

@Mkuu Malkiory: Nakubaliana kabisa na wewe!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP