Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kutokuwa na UHAKIKA labda ni kitu KIZURI pia,....

>> Friday, May 27, 2011

 ......hasa KWA KUWA ,...
....WENYE UHAKIKA inasemekana kwa kawaida HUCHELEWA kustukia jinsi,....
.....YASIVYOKUWA na UHAKIKA yale waaminiyo WANAUHAKIKA nayo!:-(


Swali:
  • SI ulishasikia wataalamu wa enzi hizo waliokuwa na UHAKIKA kuwa DUNIA iko BAPA kama MEZA hasa wale wa KANISA LA ROMA  ilivyowahikuwachukua MUDA SANA kukubali  kuwa DUNIA ni ya DUARA kisa walikuwa na UHAKIKA?
  • Na siunajua jinsi iwezavyo kuwa vigumu kumkubalisha MSABATO kuwa labda WAKATOLIKI wa KIROMA wako sahihi na DOGMA zao kwa kuwa KISABATO wana UHAKIKA au tu kwa kinyume chake- bila kusahau iwezavyo kuwa vigumu kuwahakikishia WAISLAMU kuwa  kwa kuwa WASABATO nao hawali NGURUWE labda basi hao ndio WAKO sahihi KIKRISTO  kwa kuwa  KIISLAMU wanauhakika?

  • Kwani UNAUHAKIKA ambao ushawahi kudumu bila hata tetesi za wasiwasi kwa mbaaali wakati fulani  hata kama hapa tunaongelea UJUAYO na sio tu mahusiano yako na mpenzi au kuchamba vizuri?

Ndio,..
.... katika maswala ya UHAKIKA wa NDUDE,...
..... ingawa  kuchelewa KUSTUKIA  kunaweza kufanya uwe FARAJANI MUDA MREFU huku UMERIDHIKA kwa kuwa unauhakika na kwa hilo hata katika mahusiano kukatunza mpaka ndoa ya  MTU MWENYE UHAKIKA kwa muda ZAIDI,...

.... lakini  labda pia bado ni KWELI  kuwa awaiye kustukia  KITU kwa kuwa tokea awali alikuwa HANA UHAKIKA kunaweza kuokoa MTU ,...

... na hata kama hapa HATUONGELEEI kujiokoa kwa MTU  kwenye NDOA YAKE  na MAAMBUKIZI ya NDANI YA NDOA kwa kuwa  kutokuwa kwake na uhakika kumefanya astukie mapema  MWENZA WAKE katika NDOA anakamchezo kakudokoadokoa  nje ya ndoa.:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Na nakutakia IJUMAA na WIKIENDI  KIBONGE Mwanakwetu !


Hebu DUB FX atufix-RUDEBOY



The Streets walainishe kwa - Could Well Be In



Au turudi tu MADAGASCAR ili Songo Love waletete-Ngoma MAMA



Nafikiri labda tubakie tu hapahapa MADAGASCAR ili ROSSY alete tu naye  kitu-Ino Vaovao


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 12:53 am  

Katika mapenzi unatakiwa uwe na uhakika, Ndugu yangu... hata kama ni uhakika wa bandia. Kama sivyo,huwezi ukajenga nyumba!

Yasinta Ngonyani 1:47 am  

Kaka Mkubwa Phiri umenena haswa:-) Simon hata mie naona umefanya vizuri kuishia hapa madagascar maana patamu kweli...:-( au :-)

Simon Kitururu 11:03 am  

@Mkuu Goodman: Kwani UHAKIKA na UHAKIKA wa bandia ni kitu kilekile?

@Yasinta: Kuhusu Madagascar:-)

Yasinta Ngonyani 2:52 pm  

Simon mbona unatabasamu kuhusu Madagascar nimekosea kwa kusema hivyo au? Na hapo kaka mkubwa Phiri naona anataka kusema kuna mapenzi ya dhati na kuna kule kupenda kwa kudanganyana ....kumwambia mwednzako maneno matamu halafu kumbe ni uwongo tu..kaka Phiri upo?

Simon Kitururu 2:58 pm  

@Yasinta: Kuhusu tabasamu la Madagascar nimekumbuka tu ndoto fulani!:-)

Kuhusu Mkuu GOODMAN nilivuyomuelewa mimi ni kuwa anasema usipokuwa na uhakika huwezi kumuamini hata mwenza wako ambaye bila yeye mahusiano kama Baba na Mama wa NYUMBA hayatawezekana.

Kitu kilichofanya nihoji kama UHAKIKA wa bandia au wakujilazimisha kama unawezekana ,...
... na na ndo maana nikauliza kwani UHAKIKA bandia na UHAKIKA wa KIKWELI ni kitu kilekile au la!

Mapenzi ya dhati yapo na mapenzi ya KUDANGANYANA labda hayapo kama wote wawili katika penzi wanadanganyana kwa kuwa hilo halitakuwa penzi tena,...
... ingawa MAPENZI ambayo mmoja anadanganya na mwingine kapenda kikweli yapo pia!:-(

Yasinta Ngonyani 3:07 pm  

Ndoto fulani kuhusu madagascar ok:-)
Naona hapa nimwachie kaka Phiri nisije nikamwaga uongo bure....... nanukuu "ingawa MAPENZI ambayo mmoja anadanganya na mwingine kapenda kikweli yapo pia!:-(" Mapenzi inabidi wote wapende sio mmoja tu!!

Goodman Manyanya Phiri 10:26 pm  

@Simon
@Yasinta

Yasinta amenielewa vizuri sana; hata Simon vile aliposema [wakiwa wote wawili wanadanganyana] lakini Mkuu Simon ndipo kaishiwa na nguvu ya kimawazo ya kunielewa papo hapo, wakati Dada Yasinta alisonga mbele na kunielewa zaidi.


Kusema ukweli nilikuwa sitaki kuwashtua wasomaji wa blog yake Mtakatifu Simon LAKINI UKWELI NI KWAMBA MAPENZI YA DHATI HAMNA DUNIANI...


...Mpaka hapo akijitokeza mwanaume au mwanamke mmoja wote wasomi na watu wenye pesa zao wamvute hohehahe (tena kichaa) anaenuka uchafu akiwa anakula kwenye pipa la taka na wafunge naye ndoa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP