Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa KUNA watafutao MPENZI wampitao afaaye kuwa MPENZI kila siku kwa kuwa hafanani na WAWAZACHO wakati wanampita!

>> Friday, May 06, 2011

Ndio,...
.... hata kama sasa hivi una umuitaye MPENZI,...
... lakini labda ambaye angekuwa ni MPENZI WAKO wa KIKWELI yule BOMBA KIVYAKO ulishampita bila KUMSTUKIA njiani hata wakati ule labda ulichokuwa unafikiria ni kuharakisha kwenda CHOOONI!:-(


Na tukiachilia MBALI tunayofikiria MENGINE,...
.... yawezekana hata kama tunachofikiria ni KIPENZI inawezekana tulichojifunza kutambua kuwa ndio KIPENZI kinaathiri  uwezo wa kustukia WA KWELI mpenzi kwa kuwa hafanani na tulichojifunza ndio MPENZI!:-(

Swali:
  • SI mpenzi anaweza kuwa MCHICHA wakati sisi tumejifunza kuchagua MPENZI kwenye nyama na kujikuta maishani tuitacho MPENZI ni ile nyama ya NGURUWE?



Ndio,..
.....YETU,...
.... mara nyingi HATUYASTUKII,... 
.....na tuliyonayo ni yale MAISHA yasababishayo TUYANG'ANG'ANIE kwa kuwa hayo angalau tumejifunza kuyasikia na kujisikia ni YETU!:-(

Swali:
  • SI unajua ili kitu kiwe CHETU inabidi ujisikie kinamna fulani na ujifunze kitu fulani na ndio maana mara nyingi  waliojaribu UJAMAA na kutaka watu wajisikie ni YAO ilishindikana kwa kuwa KITU CHETU hakikufanya watu wajisikie ni CHAO na ndio maana sasa hivi UBEPARI kwenda mbele kwa kuwa angalau  KIUBEPARI inaeleweka CHETU ni CHANGU?


  • Na siunajua KUSTUKIA CHAKO labda  ni BAHATI na tuitavyo VYETU labda ni kwa kuwa tu  tumajifunza tafsiri ya KUMILIKI ni nini kitu kitusahaulishacho kuwa labda hakuna BINADAMU amilikiye kitu hapa DUNIANI na ndiomaana BINADAMU akifa  anaanza bila AVIMILIKIVYO?

  • Je unafikiri BINADAMU anamiliki hata ROHO yake?

Ndio,...
.... vingi ni MPAKA vifanane na wazo lako ndio UVIELEWE,....
... kitu kiwezachokuwa kinafanya VYAKO KIKWELI ambavyo havifanani na mawazo yako kwenye vitu HUVISTUKII,....
... kitu kifanyacho hustukii hata MPENZI wako akupitaye kila siku akikuchekea!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI njema MKUU!

Hebu kikutubadili wazo FIRST LADY abugidaun...


Au tu MAJEK FASHEK arudishe usiriasi kwa-I am not TIRED

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 2:25 pm  

Mkuu wakati nasoma hii mada ya leo, nikakumbuka methali hizi; KIPENDA ROHO HULA NYAMA MBICHI...Baadaye nikakumbuka na hii, MPENDE AKUPENDAYE, ASIYEKUPENDA ACHANA NAYE...Mhh, sijui kama ninaenda na mada hii. TUPO PAMOJA MKUU!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP