Leo katika KISWANGLISH: You know when I was in MAKERERE ndio pale nili kutana na Miss LAWINO na kujua KURIDHIKA hufanya life cheap aisee!
>> Tuesday, May 03, 2011
You know life BWANA is very cantankerous na usipokuwa muangalifu aisee unaweza kujikuta unahangaika maisha yako yote bila kuwa satisfied yani!
Inabidi ujijue wewe na insecurities zako yani kama unataka life isiwe expensive kwa kuwa unaweza kustukia moja ya kifanyacho maisha ni ghali ni katika tu kulipia insecurities zako ambazo zinaweza kujitokeza kwa nini unanunua cha ghali ili angalau u feel you are somebody -kuanzia nguo, magari, nyumba nakadhalika .
Na nilijifunzia hicho pale MAKERERE aisee na unajua enzi zile hasa baada ya kukutana na Miss LAWINO ambaye alikuwa msichana very smart kuanzia kwenye ubongo mpaka kwenye macho yake ya gololi na mashavu ya kumimina.
Msichana yule iko simple bwana na haina makuu na akili - utafikiri kutumia akili kwenye dictionary wameweka picha yake.
Yani those days wee acha tu! Yani kutokana na yeye ndio nikajua kuwa:
Oh Miss Lawino halafu sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye London wakati naenda Paris kuchekiwa meno kabla ya kurudi hapa Kigoma kwa ajili ya hii project!Musichana ile inaongea Kiingereza kama vile ni Queen Elizabeth yani!
- SI umestukia lakini jinsi inferiority complex na insecuritie katika MAISHA vinavyoweza kuwa ndio chanzo cha kuingia gharama zisizo na mpango hasa kwa ajili ya watu katika hii ku overcompansate?
Tahadhari: Leo katika KISWANGLISH:
...ni kipengele cha kuwaenzi wasomi wetu TANZANIA ambao moja ya kukutambulisha wameenda shule ni jinsi wachanganyavyo KISWAHILI na Kiingereza hata kwenye hotuba zao VIJIJINI wakati wanaomba kura kwa wanakijiji ambao labda hawakwenda shule ukizingatia halihalisi ya uchumi ilivyo Tanzania!:-(
Swali:
- Na ni kwanini naandika kipengele hiki kuwaenzi hawa wanaoharibu KISWAHILI?
- I donti noo!
- Lakini si ni tabia nzuri labda kuwaenzi Waheshimiwa?
Na kuwaenzi hawa wasomi wetu labda tuwapigie tu wimbo wa kiingereza ..
na nahisi Welcome To My World kutoka kwa - Jim Reeves unaweza kusaidia hilo
Au tu angalau wimbo wa X-mass hata kama ni katika kipindi cha majira ya PASAKA hasa kama santuri yenyewe iliyopo nyumbani kwenye radio gram ndio hiyohiyo ya X-mass.
Au tu The Mighty Sparrow wabadili kidogo na kututoa eneo fulani kiwazo kwa -Good morning Mr. Walker
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment