Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Haki za MZAZI wakati MTOTO wa MZAZI kashafikia UKUBWANI!

>> Sunday, May 22, 2011

LABDA ni vigumu kwa MZAZI,..
... kuanzia KUJIFUNZA mtoto wake ANAWAZA NINI,...
... wakati MTOTO WAKE  yuko tayari UKUBWANI!:-(

Swali:
  • AU?

Na wakati  MZAZI anakimbilia kumfinya MTOTO WAKE wakati mtoto ni mdogo ,..
....kwa kuwa kanya pembeni ya CHOO,...
..... inaweza kuwa ni kosa  kama MZAZI hakujaribu kujua ni nini hasa sababu mtoto wake anajikojolea kitandani-SAMAHANI - nilitaka kusema  - ni kosa kama MZAZI hakujaribu kujua ni nini HASA sababu kwanini mtoto wake hakulenga silaha ya MAVI kwenye tundu la CHOO kabla MZAZI hajamfinya, KUMGOMBEZA au hata kumpiga bonge la MBATA kabla fimbo haijaletwa ili MTOTO achapwe ili ashike adabu kwa kitu ambacho labda siri yake MZAZI hajachukua muda hata kuijua,...
... kwa kuwa tu kwa UKUBWA WA MZAZI kama MZAZI - mzazi anafikiria tu kuwa ,...
.... kwenye shimo la CHOO  ambalo ni mwiko hata kwa tone la MKOJO kuleta unyevunyevu pembeni na   ni kujambia tu pembeni ya shimo la choo kuruhusiwako kwa WASTAARABU,...
... iweje MTOTO huyo wake KIBONGE anye pembeni!:-(



Swali:
  • Si unajua labda siongelei MAVI wala CHOO kwenye taralila hii?
  • Kwani hujui ni WAZAZI wengi tu hawaelewi WATOTO wao kisa hawachukui muda kujiweka katika mazingira ya watoto wao na kufikiria ni kwanini WATAKAVYO kama WAZAZI na WAWAZAVYO kama WAZAZI labda  haviendani kabisa na wafikiriavyo watoto hata kama labda ni kweli watoto wasingetakiwa kufikia mpaka kunya pembeni ya choo ili  WAZAZI wastukie chakula wawalishacho hakiyeyuki kwenye tumbo la mtoto ndio maana kinyesi kimejaa mahindi na miba ya samaki ambayo tumbo la MTOTO  limeruka kuyayeyusha?

Ndio,...
...tukiachana na yote,...
... labda kama wewe ni MZAZI ,...
... labda jifunze kumsikiliza mwanao tokea utotoni,...
... kwa kuwa haki ya nani unaweza kumjulia jinsi ya kumuadabisha vyema HATA BILA KUMKWIDA KIBINDO na kupunguza uwezekano wa kuabishwa na toto lako hata lile lenye kichwa kama tofari likishafikia UKUBWANI!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu turushwe na Kris Kross katika-Jump


Au tu Kriss Kross waje na Supercat warudie- Alright

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:22 pm  

Kwanza nasema ahsante sana nimelipokea wazo lako kaka Simon wa mawazomawazo...

Goodman Manyanya Phiri 8:35 pm  

Unaambiwa na wanasaikolojia usimwazie mtoto anawaza nini kwani wewe mzazi wa mtoto sio mtoto wako kamwe!

Simon Kitururu 10:26 pm  

@Mkuu Goodmana: Nasikia kwa kuwa Wanasaikolojia ni BINADAMU kuna wadaio hiyo ni sabababu kubwa kuwa labda WANASAIKOLOJIA hawajui kila kitu:-(

@Mrembo Yasinta:Mmmmh!:-(

emu-three 10:14 am  

Swala la uzazi na matunzo ya mtoto kweli yana sheria au utaratibu ambao kila mzazi anatakiwa kuufuata ili mtoto wake awe `hivyo'
Hapo kulenga shimo umeangalia `akina sisi' je wale wanaotumia choo cha kuflash...labda tuseme kanya hajaflash, kwanini?
Kwa ufupi kama mzazi anawaza sana jinsi gani mtoto wake akue katika maadili anayopendezewa nayo, lakini kipindi hicho cha kutafakari na kumueleimisha..kinakuwa kifupi sana ukizingatia kuwa mtoto akishakuwa anachanganyikana na jamii...je utafanyaje ili akusikia wewe, na ayaponde yale ya wanajamii wengine...muda unakwenda ukiwaza, mtoto anakuwa...mara utandawazi unachukua nafasi yake...anajua kunywa kuflash, kutumia toilet paper...sasa wewe wamletea choo cha shimo, na kapo la kunawia,wapi na wapi...umeshachelewa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP