Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati TUNAFURAHIA mtu KAFA!

>> Tuesday, May 03, 2011

UBINADAMU una mambo yake hata  katika YALE ya,...
... ni  nani ANAHUZUNIKIWA akifa!


Na  swala la MAREHEMU alikuwa ni MTU mzuri,....
.... labda ni  jambo tu lenye udhaifu wa KIBINADAMU kama tu lile la MAREHEMU alikuwa ni MTU mzuri hasa ukizingatia kuwa kwa kuwa BINADAMU wana udhaifu wa KIBINADAMU hata katika swala zima la KUJUA,.....
.... labda mambo mengine tumuachie MUNGU ajuaye yote hasa katika  kuhukumu.:-(




Swali:
  • SI inasemekana hata kwa waaminio MUNGU ni MUNGU pekee ndio anajua MAREHEMU alikuwa na ubaya au uzuri gani  KIUHAKIKA na kaenda mbinguni au MOTONI  ?
  • SI umestukia BINADAMU washangiliavyo katika BAADHI ya misiba na KULIA sana  kwenye ile mingine misiba wakati labda watumiacho kujenga MAFILINGI labda ni wayajuayo KIBINADAMU tu  na yenye UDHAIFU wa KIBINADAMU?

  • SI labda kuna uwezekano HITLER na Osama BIN LADEN wako mbinguni ingawa KIBINADAMU kuna wadhaniao wanajua kuwa hawa jamaa walikuwa watu wa BAYA?

Ndio,....
...... wakati tunahuzunika MTU kafa,...
.... tukumbuke labda tusingefikiria FIKIRA zenye udhaifu wa KIBINADAMU labda tungestukia ,...
.... labda MAREHEMU kapumzika!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA,...
....ambalo limepewa mimba na jinsi watu wafurahiavyo kifo cha mtoto mtundu Osama Bin Laden!:-(



Katika uchokozi...



Au tubadili tu kidogo kwa hii mash up ya Ain't That Peculiar ya Marvin Gaye na Summer Madness ya KOOL & the Gang





Au tu James Mtume aje na kundi zima la  MTUME wadai - You me and He


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:44 am  

Nanukuu "SI labda kuna uwezekano HITLER na Osama BIN LADEN wako mbinguni ingawa KIBINADAMU kuna wadhaniao wanajua kuwa hawa jamaa walikuwa watu wa BAYA?


Ndio,....
...... wakati tunahuzunika MTU kafa,...
.... tukumbuke labda tusingefikiria FIKIRA zenye udhaifu wa KIBINADAMU labda tungestukia ,...
.... labda MAREHEMU kapumzika!:-(" mwisho wa nukuu.... Inawezekana ni kweli na inawezekana si kweli....

Simon Kitururu 7:05 am  

@Yasinta: Mmmh!

Yasinta Ngonyani 7:41 am  

Mt. Simon kwanni unaguna nimekosea?

Simon Kitururu 8:14 am  

@Nangonyani: Hujakosea!Kuguna ni moja ya tabia zangu mbaya tu katika kujulisha watu nimesoma walichoandika !:-(

Yasinta Ngonyani 8:39 am  

Mmmmh! Ahsante kwa kufafanua maana ya hii Mmm!...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP