Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

R.I.P marehemu wote wa MV BUKOBA!

>> Saturday, May 21, 2011

Tarehe kama ya leo MELI ya MV BUKOBA ilizama katika ZIWA NYANZA lijulikanalo pia kama Ziwa Ukerewe, The Eye of the Rhino, Nalubaale, Sango, Lolwe,...

....au tu tubishe tusibishe,...
...Lake VICTORIA!

Na chakusikitisha ni kwamba nasikia matatizo yaliyofanya MV BUKOBA izame yako tu palepale kwenye meli karibu zote kwenye Lake VICTORIA leo hii , Lake Tanganyika LEO HII kama alivyowahi kutoa ushahidi CHIB wa Blog ya HADUBINI .....na hata lake NYASA/ Lake MALAWI [...wakati jina Ziwa MALAWI ni kwa kuwa MALAWI wanajua lote ni lao,...
....na MSUMBIJI nao sina uhakika sana ingawa nasikia nao wanaliita LAKE MALAWI,...
wakati TANZANIA wamekaa kimya kitu kifanyacho Tanzania kusini hakuna mpaka ujulikanao kiuhakika KIMATAIFA :-(]


Ngojea niache longolongo,...
.....R.I.P wote mliotokwa roho kwenye M.V. Bukoba siku yenye TAREHE hii 21 May 1996!


Nimewakumbuka!:-(


Hebu tupate kitulizo kutoka kwa Rose Muhando akidai - Nipe Uvumilivu



Rose Muhando adai zaidi -Mungu Wangu nitakushukuru




Au tu ZAIMO ahamishe wazo zima ILITUANZE UPYA  huku akidai-MUNGU akipenda

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

hansom 11:09 am  

Ajali hii itukumbushe vyema kukagua meli zetu ili tujiepushe na majanga mengine yanayoweza kutokea,Mungu awaweke mahala pema peponi roho za marehemu wote, Amina.

EDNA 11:46 am  

Mungu na azilaze roho za marehemu wote peponi.

Yasinta Ngonyani 8:38 pm  

Mungu zilaze roho za marehemu wote peponi. Amina.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP