Umuhimu wa kuwa wa MWISHO kwa mtu wa MWISHO!
>> Wednesday, May 25, 2011
MTU wa MWISHO,....
....labda ni MUHIMU sana kwa swala zima la kujisikia vizuri kwa ashangiliaye sana kwa kuwa WA KWANZA,.........kwa kuwa labda hakuna wa kwanza kama hakutakuwa na wa MWISHO!:-(
Swali:
- Na si inasemekana ni DALILI ZA UDHAIFU FULANI hata katika kitengo cha kujiamini kwa MTU WA KWANZA kama anafarijika sana na kitendo cha kuwa WA KWANZA?
Na kwa kuwa kwa bahati mbaya JAMII inafunza wanajamii kuthamini zaidi WA KWANZA ,...
..... kuwa WA PILI huanza kufikiriwa kama ni MWANZO wa KUSHINDWA.:-(
Na cha kusikitisha ni kwamba katika jamii huwa kuna baadhi husahau kuwa katika kitu fulani kwa mfano umalaya - MTU WA KWANZA,...
....labda ni katika kitu fulani tu NI WA KWANZA na huyo huyo kwenye kitu kingine kwa mfano katika TAALUMA YA kupiga chabo -huyo huyo WA KWANZA kwenye ya KEMIA kwenye WASHINDI wa HESABU anaweza kuwa ndiye anayeSHINDWA.:-(
Swali:
- Lakini si labda isisahaulike kuwa- KUWA WA MWISHO kuna umuhimu wake na kama umuhimu huo hauko sana kwa WA MWISHO basi angalau uko kwa wengine hasa katika JINSI WANAVYOJISIKIA walioko kwenye shindano?
- Na si inasemekana USHINDI ufanyacho kikubwa ni kufariji tu kwa muda WALIO amini WAMESHINDA hasa kwa kuwa inasemekana wengi watoao zawadi kwa washindi ni wale isemekanao kuna kitu HAWAKUSHINDA?
Ndio,...
.... kwa kuwa kama kuna WATU WAWILI,...
.... basi wa pili katika kidedeo ndiye WA MWISHO,...
....basi kama kuna mtu mmoja labda wa kwanza ndiye wa MWISHO!
Ni wazo tu hili na usikonde MHESHIMIWA!:-(
Hebu Ayo aingilie kati kwa - Lonely
Ayo aendeleze kwa - Slow, Slow (Run Run)
Au tu Irma atulize kwa - I know
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Haswa wa kwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza:-(
@Yasinta
Msemo wako huo unakujaje sasa katika mandhari hii?
Nitakupa jibu!!
Nikutokana na kwamba yule wa kwanza ni kifutio tu cha machozi ya wale waliojaribu kwa bidii labda kuliko yeye lakini wakashindwa kufanikiwa kuwa wa kwanza.
Watarudia bada ya kushindwa kwao, hakika! Na siku watakaposhinda nao, watafanya siyo tu makubwa kuliko yale yake wakwanza aliyeyafanya, bali wataweza hata kumkosoa kama ni wa kwanza kibandia tu.
Kifupi, usijidai sana kama wewe ni wa kwanza; na nafikiri Dada yangu umenukuu vizuri sana uliposema "wa kwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza".
Post a Comment