Leo katika UCHOKOZI: Wakati tunaona picha za RAIS OBAMA akiwa kwa ndugu kule IRELAND unafikiri ni kwanini hajakanyaga KENYA tokea achaguliwe kuwa RAIS wa MAREKANI?
>> Tuesday, May 24, 2011
Rais OBAMA tunajua aliwahi kusema:
"It never hurts to be a little Irish when you're running for the presidency of the United States of America" .
Swali:
- Does it somehow hurt a little to be Kenyan when you're running for the presidency of the United States of America?
Tucheki akiwa Ireland tena....
Kwa uchokozi zaidi tupate uchokozi zaidi....
NI UCHOKOZI TU HUU MHESHIMIWA na wala USIKONDE!
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mmmh...hili nalo neno @ Mtakatifu, labda anasubiri akishinda tena kwa awamu nyingine atakwenda kutambikia...lol!Ila naona kama jamaa yuko proud kunasibishwa na Wa-Irish kuliko Wakenya!
Kama tulivyofanya kwa uAfrika wake huyu jamaa kiasili, nao uIrish wake tunaweza kuupanua kuliko inavyostahili.
Mtu akisema "Nampenda Yesu", usidhanie kwamba lazima atamchukia Shetani, kwani haki za mtu asiekuwepo wakati Mola alipoanza kugombana na Ndugu yake Lucifer/Shetani, zimehifadhiwa na kusalamishwa kisheria hata za huko Mbinguni!
Lamwisho kutoka kwangu, Obama siyo Mwafrika wala Mu-Irish. Huyu ni Mwamerika kwisha. Tutakuja kutapeliwa bure hapa tukiendelea kukimbizana na rangi ya ngozi ya mtu au jinsi nywele zake zilivyokaa...upumbavu mtupu (kwa maoni yangu, lakini).
Afrika, Amkeni Usingizini!!!
@Mwanasosholojia:Inawezekana lakini ni MEDIA tu zituuziavyo habari ndio tujengavyo mitazamo katika hili lakini!:-(
@Mkuu Goodman:Umenena Mkuu!
Post a Comment