Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa WAMPENDAYE hata HITLER wale WATU, labda hujitahidi KIRAHISI kukumbuka yake MAZURI tu ya MTU!

>> Tuesday, May 24, 2011



Na kwa kuwa WACHUKIWAO,...
.... mazuri yao HUSAHAULIKA kirahisi,...
.... bado labda ni KWELI hakuna AKUMBUKWAYE kwa MAZURI ambaye hana MABAYA YAKE kama baadhi ya wapenzi wa Rais NYERERE wapendavyo kuamini,...
... kwa kuwa haki ya nani MBAYA yeyote kwako anamazuri yako hata kwako na moja ya sababu huyaoni labda ni kwa kuwa umeamua tu ki chuki na miasira yako kutotaka kustukia kuwa kuna upande wa pili wa kila SHILINGI!:-(

Swali:
  • AU?

Ni wazo tu hili KAMANDA!:-(






Hebu Meiway atupe-Adibebe



Meiway aongezee dozi akiwa na Koffi Olomide katika ndude-KK MOU Prudencia


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:39 am  

Hii ni kawaida mtenda hakumbuki bali mtendewa ndiye anayekumbuka:-(

Unknown 1:28 pm  
This comment has been removed by the author.
Unknown 1:47 pm  

Ngoja nikukumbushe moja ya POST yako ya Thursday, June 14, 2007
UNAKUMBUKA ULIPOANZA KUPENDA?

........Ukaendelea:

Duh!
Samahani!

Nafikiri nilitaka kuuliza hivi:

* Unakumbuka ulipoanza kuchukia?


Inasemekana watu wengi hukumbuka walipoanza kupenda kuliko walipoanza kuchukia, lakini wanachukia kirahisi kuliko kupenda.

Si unajua tena!Historia ya kupenda inasemekana ni rahisi kuikumbuka au hata kuiimajini kuwa tunakumbuka. Si unajua tena vile vimaswalaa....!:

* Wengi wetu cha kwanza kupenda ilikuwa nyonyo ya mama.

* Kupenda kale kadoli!

* Kumpenda rafiki fulani pale utotoni!

* Hata kale kamwanzo kakuanza kumpenda mwanadada fulani au mwana kaka fulani.......

* Nakadhalika kadhaaa wa kadhaa.......

* Kupenda msosi fulani!

Lakini ukweli ni kwamba moja ya tendo la binadamu alifanyalo akizaliwa tu, ni kuchukia.
Akizaliwa tu halafu yuko hai , atalia kuashiria kuwa kashastukia bughudha za ulimwengu.Kachukia kakitu ambako siye tumekazoea!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP