Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WATOTO wa TANZANIA kuzidi kujilea wenyewe !

>> Thursday, May 26, 2011

Ukiachilia WATOTO yatima,....

..... na watoto wa mitaani wale waonekanao mitaani wakijitegemea kwa kufanyakazi  kama zile za OMBAOMBA na kadhalika KADHAA  ili kulisha familia,....

...... inasemekana katika KUNDI la WATOTO WANAOJILEA WENYEWE sasa hivi wanaingia pia watoto wa kwenye FAMILIA zenye kulimbukia MAMBO yaitwayo ya KISASA yenye mrengo wa KIMAGHARIBI,...

.... ambao  hata kugombezwa hawagombezwi na HUCHUKULIWA kama WANAJUA kila kitu na ndio maana KUBISHIA WAKUBWA au hata kuwatusi kidogo KWAO  ni ruksa bila kusahau pia kwao ni  nadra kukutana hata na wazazi wao katika mkao wa kujadili MAMBO KWA KINA  kisa WAZAZI wako BIZE!:-(

Swali:
  • Kwani hujastukia hilo?


Na kama hili ni kweli, ....
....na jinsi ionekanavyo ili kieleweke KIMAISHA kila MZAZI  hata asiyemaindi UMAGHARIBI/Mambo yaoanishwayo na WAZUNGU katika TANZANIA hasa mijini,...
...itabidi AZIDISHE muda wa kufanya kazi kama akibahatika kupata kazi TANZANIA,...
.... kuna tetesi sio miaka mingi ijayo  WATOTO wa TANZANIA kwa kiwango kikubwa KABISA watakuwa WANAJILEA WENYEWE kwa kuwa WAZAZI hawana MUDA wa MALEZI ya WATOTO na SERIKALI haina uwezo wa KUSAIDIA watoto walelewe kama WATOTO!:-(


Swali:
  • Unaweza kubunia TANZANIA itakuwa NCHI ya aina gani ifikiapo WATOTO waliojilea WENYEWE ndio wameshika hatamu?


NI mtazamo tu HUU kiwazo baada ya jambo kustukiwa!


Hebu tugewe Kwela music kutoka kwa Spokes Mashiyane akitupa - Kwela Kong



Au tu Spokes Mashiyane atugee dozi zaidi ya Kwela katika pia  pia kitu  - Meva





Kabla Mafikizolo ft Hugh Masekela hawajarudia - Kwela


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP