Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

R.I.P Sheikh Yahaya HUSSEIN mtabiri maarufu TANZANIA !

>> Friday, May 20, 2011

Kutokana na vyanzo vyangu vya habari kutoka BONGO NYOSO,...

Mheshimiwa Kafariki DUNIA leo asubuhi nyumbani  kwake Magomeni, jijini Dar es Salaam.!:-(



Tukiacha mengine,...
....AKSANTE kwa UTABIRI na mengi mengine yaliosaidia watu  katika MAISHA YAKO!


Mie BINAFSI nilikuwa nazimia SANA TU jinsi CHOCHOTE usemacho kisumbuavyo akili  hata WAJANJA!:-(

R.I.P Sheikh Yahya!








Hebu tugewe Shukran Allah na Kurbaan



UPDATE: 
Nje ya habari zangu za kiintelijensia kutoka kwa majirani zake,...
....Source mpya ambayo ni: Radio Free Africa,....
...imedinya hewani pia habari HIYOHIYO  kimkao huohuo!.

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:20 pm  

Marehemu astarehe kwa amani. Amina.

malkiory matiya 3:06 pm  

Rest in peace! kifo ni mwisho wa yote, marehemu alikuwa bingwa wa kutabiri vifo vya viongozi wa kisiasa, japo utabiri wake haukuwa sahihi wakati mwingine. Lakini sijui kama aliweza kutabiri juu ya kifo chake mwenyewe!

emu-three 3:47 pm  

R.I.P! Ndio maisha yalivyo, kuwa kila mmoja ni mtarajiwa, hatunz azaidi ila kumuombea kwa mola!

Anonymous 4:00 pm  

kifo chake kinafunga mlango wa giza nene la kuongoza nchi tukufu ya tanzania kwa uchawi na ramli. kinafunga milango ya minyororo ya imani potofu. kinafungua mlango wa nuru ya ujio wa taifa jipya la tanzania lenye watu wamwaminio mungu wa ukweli. taifa litakalokuwa na kuheshimiana kusikokuwa na vitisho vya 'atakufa fulani'. ni taifa la namna hili ndilo linaweza kustawi.

mungu amuweke mnajimu pahala anapostahili kuwekwa.

chib 9:40 pm  

RIP Shaikh.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP