Moja ya sababu kuna SINDIMBA, MDUNDIKO, bongo fleva , MIPASHO , taarabu na LUBOGOBOGO,...
>> Monday, May 23, 2011
... ni kwa sababu BINADAMU hupenda kubadili asili ya viwasikilizacho utamu,....
.... na BINADAMU wapendao utamu uleule hujiakikishia wanapenda UTAMU huu na sio ULE kwa uwepo wa utamu wa aina nyingine!:-(Swali:
- SI nasikia wapenda MAANDAZI wasingekuwa na uhakika na mapenzi yao ya MAANDAZI kama kusingekuwa na vitafunio vingine?
- Na si inasemekana kila siku MAANDAZI na chai tu huweza kufanya mtu aingie hamu ya angalau siku moja moja aonje VITUMBUA?
Kwahiyo,....
.... kama unalimpenzi LAKO na siku mojamoja unatulizia penzi sehemu nyingine ,...
.... ufanyacho KIBINADAMU ni kitendo kinachoruhusiwa kwa kuwa kinaleta maana kibinadamu,...
...BINADAMU ambaye kwa kawaida kaumbwa makusudi na uwezo wa kutofautisha aina mbalimbali za TAMUTAMU,....... hasa kama IMANI zako haziingilii kati kukutoa uhuru wa kufanya uwezayo KIBINADAMU ambayo sio MENGI kihivyo!:-(
Swali:
- SI umestukia BINADAMU kwa udhaifu wa KIBINADAMU ni mengi hawawezi kufanya halafu wawezayo kufanya hujitungia sheria na MAADILI yafanyayo na wawezayo kama vile yale ya udowezi wa yasiyo yao WASHINDWE kuyafanya?:-(
..... labda kuna sababu kuwa ingawa SINDIMA ni ngoma nzuri,...
.... KIBINADAMU bado na MDUNDIKO upo na wahitajika!:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Ukifanikiwa inasemekana ndugu hujitokeza !
Ngojea tutembelee ndugu za Rais Obama huko Ireland
AU hebu Hugh Masekela achokoze tena...
Hugh Masekela aendelee....
Au tu MUTABARUKA akatizie denge na kudai -SIT DUNG PON THE WALL
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment