Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Moja ya sababu kuna SINDIMBA, MDUNDIKO, bongo fleva , MIPASHO , taarabu na LUBOGOBOGO,...

>> Monday, May 23, 2011

... ni kwa sababu BINADAMU hupenda kubadili asili ya viwasikilizacho utamu,....
.... na BINADAMU  wapendao utamu uleule hujiakikishia wanapenda UTAMU huu na sio ULE kwa uwepo wa utamu wa aina nyingine!:-(

Swali:
  • SI nasikia  wapenda MAANDAZI wasingekuwa na uhakika na mapenzi yao ya MAANDAZI kama kusingekuwa na vitafunio vingine?
  • Na si inasemekana kila siku MAANDAZI na chai  tu huweza kufanya mtu aingie hamu ya angalau siku moja moja aonje VITUMBUA?


Kwahiyo,....
.... kama unalimpenzi LAKO na siku mojamoja unatulizia penzi sehemu nyingine ,...
.... ufanyacho KIBINADAMU ni kitendo kinachoruhusiwa kwa kuwa kinaleta maana kibinadamu,...
...BINADAMU ambaye kwa kawaida  kaumbwa makusudi na uwezo wa kutofautisha aina mbalimbali za TAMUTAMU,...
.... hasa kama IMANI zako haziingilii kati  kukutoa uhuru wa kufanya uwezayo KIBINADAMU ambayo sio MENGI kihivyo!:-(

Swali:
  • SI umestukia BINADAMU kwa udhaifu wa KIBINADAMU ni mengi hawawezi kufanya halafu wawezayo kufanya hujitungia sheria na MAADILI yafanyayo na wawezayo kama vile yale ya udowezi wa yasiyo yao WASHINDWE kuyafanya?:-(
Ndio,....
..... labda kuna sababu kuwa ingawa SINDIMA ni ngoma nzuri,...
.... KIBINADAMU bado na MDUNDIKO upo na wahitajika!:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(



Ukifanikiwa inasemekana ndugu hujitokeza !
Ngojea tutembelee ndugu za Rais Obama huko Ireland

AU hebu Hugh Masekela achokoze tena...


Hugh Masekela aendelee....


Au tu MUTABARUKA akatizie denge na kudai -SIT DUNG PON THE WALL

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP