Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama hupendi KUZEEKA-``HONGERA za SIKU YA KUZALIWA labda ni MATUSI aisee!´´

>> Wednesday, October 05, 2011




Swali la KIZUSHI:
  • Kwani  MTU huwa anapongezwa nini katika BIRTHDAY ukizingatia labda hana mchango wowote katika kufanya awepo hapa DUNIANI katika siku hiyo hasa kama unaamini katika MAPENZI ya MUNGU mwanadamu hawezi kuingilia?
  • Na je ni kwanini kuna BINADAMU hufikiria MUNGU muwezesha yote NDIYE ahitajiye KUSHUKURIWA  kwa kuachia limtu likue wakati MAPENZI yake labda ndio yaondoayo wengine MAPEMA  kisababu zake?
  • Hudhani pongezi nyingi za watu katika siku ya kuzaliwa MTU labda ni kukosa chakusema?

Ndio,...
... labda si kwa kila MTU ni furaha MIAKA kuongezeka,...
.... hasa kwa kuwa MIAKA kuongezeka ndio siri ya UZEE,..
....ambao sio kila mtu yuko huru nao KIHIVYO.

Swali  zaidi kizushi:
  • Kwani wewe unapenda KUZEEKA?
  • Si nasikia kuzeeka kwa mpenda UZINZI huja na MZINZI kushindwa kuendelea kujinoma KIZINZI kirahisi?
  • Na si kuna waaminio MIAKA izidivyo mvuto wa MREMBO hunywea na sio kwa titi tu kulala?

Ndio,...
... umri huja na faida zake KIBUSARA,....
..... lakini  bado kuna walalamikao kwa kuwa UMRI huja na meno kung'oka kitu kifanyacho ni WAZEE wengi ndio VIBOGOYO  kitu kifanyacho mpenda KITIMOTO kushindwa kugida nyama UMRI ukienda!:-(

Na ni wazo tu hili la kizushi MHESHIMIWA!
Jumatano njema MKUU!

Hebu turudi KENYA ili Gidi Gidi Maji Maji warudie - Unbwogable



...DJ ariwaindi and come back again,...



 Gidi Gidi Maji MAJI na Wikimosh waongezee dozi kwa - Atoti



Halafu tena Eric WAINAINA amalizie na-Nchi Ya Kitu Kidogo


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP