Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi ni WATANZANIA wangapi wamewahi kufikiria kukwea MLIMA KILIMANJARO ?

>> Monday, October 10, 2011

Kuna mambo  yako tu JIRANI ,....
.... kama MUBGA za WANYAMA Tanzania au Milima ya ULUGURU,....
.... ambayo ni WAGENI  waonao thamani zake na  watambuao hata tamutamu zake kimahudhurio.

Hebu tumdeku  MGENI  akijipima  kwa kukwea ndude ya BONGO,...
... bila MIKONO wala MIGUU .....




Au tusikie ya Neil Duncan, Dan Nevins, Kirk Bauer wa Disabled Sports USA,...
... katika yao ya Mlima Kilimanjaro,....



Ndio,...
.... kuna wadaio MAISHA ni magumu BONGO,...
..... kitu ambacho tayari ni kigumu tayari na kifanyacho mengine ni ya KITALII kuwa ni LAKSHARI.


Swali la KIZUSHI kwa FISADIZ:

  • Vipi WAHESHIMIWA Fisadiz ambao labda muna MUDA na PESA, ..... mshawahi tembelea hata MIKUMI kujua angalau KIBOKO JIKE uso kwa uso anapendelea wanja ya rangi gani?
Usitishike MKUU labda nazingua tu!:-(
Jumatatu NJEMA!

13 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:47 am  

Kwa kweli leo umetoa mada nzuri sana kwani kuna vitu vingi sana ambavyo watanzania wengi wangetakiwa angalao kuona utajili tuliokuwa nao...Hebu fikiria nchi yetu lakini, wageni wanakuja na kufaidi na sisi wenyewe hakuna . Nilisikitika na nasikitika sana kuona kama pale Jangwani Sebrezz kaja mtu kutoka sijui Bangladeshi na kuweka fensi pale ili watu wakija walipie ..kweli huu ni uungwana jamani?

Simon Kitururu 10:29 am  

@Kapulya: Ndio hapoooo!:-(

sam mbogo 12:40 pm  

Niaibu Simon.mimi nimekuwa napigia debe sana mlima Kilimanjaro swali kama hilo hujiuliza nilini nita panda,jibu sijuwi. ila nina mkakati wakuanza kutembelea sehemu za kitalii Tanzania,mbuga za wanyama, na mlima kilimanjaro ila kwa sasa kupanda sina uhakika sababu ya afya( pumu) hivyo nina hitaji maandlizi makubwa. safi mkuu kwa kutukumbusha.kaka s.

Yasinta Ngonyani 2:01 pm  

Kaka S. Una tatizo la afya kwa ajili ya kuvimba tu au ni homa?...Nilisahau kusema hapo juu mimi nilianza kupanda lakini nilishindwa kufika kileleni:-(...

sam mbogo 2:14 pm  

Yasita,sijakupata,ninatatizo la kuvimba!!? au homa? nina pumu au athuma,nina wasiwasi kwa sababu imenianzia ukubwani.hivyo sina hakika naweza kupumua vizuri kutokana na hali ya hewa,umenielewa mamayangu kapulya mtoto wa ngonyani. ngoja niendelee kufikiri swali lako. asenti. kaka S

Yasinta Ngonyani 2:28 pm  

Ok, kaka S. Nilipouliza kama umevimba? Nilikuwa na maana unashindwa kupanda mlima kwa vile umenenepa mno au?..Sasa nakuelewa pole sana kwa hilo. Ila nina imani utaweza tu sio lazima ufika kileleni au?

sam mbogo 5:06 pm  

ukisika chenga ya mwili ndo hiyo uliyo nipiga.hakika siyo mnene ,ni mtu wa mazoezi sana tu na ndiyo maan pumu hii hainywewi dawa,situmii dawa inapotokea imenibana,kwa sababu tatizo nalijuwa,kuwa ni aleji nahasa vumbi hapo utanionea huruma.kwa hiyo mazoezi kwa ngu nimuhimu sana.kuna kauchokozi nimekashitukia ,mbona mimi kileleni nafika yasinta!!! .kaka s

Mija Shija Sayi 5:57 pm  

Bonge ya swali Kitururu.., hata na mimi Yasinta umenipata kwa swali lako kwa Sam...

Yasinta Ngonyani 6:20 pm  

Kumbe tupo wengi wenye aleji ...Kaka S nawe huna dogo mweeeh Kazi kwelikweli..Kilele cha mlima au kiswahili changu kimepinda?
Mija:-)

Yasinta Ngonyani 6:23 pm  

Kaka S. Nimekumbuka kitu kuwa nilikuona ana kwa ana huna mwili mkubwa ni kweli umekaa kimazoezi..:-)

Mija Shija Sayi 6:55 pm  

Yasinta kaka S ni mcheza ngoma afrika mashariki na kati hakuna..kwa hiyo mazoezi hapo yametulia..

sam mbogo 7:21 pm  

kiswahili chako kidogo kilipinda(natania) nikwambie kitu Yasinta,wewe nawenzako,mtakatifu,mija,chacha,Edina,Rachel na wengi nita wataja kesho.blog zenu zimenisaidia kunyoosha kiswahili.Da mija ngoma sasa hivi zinachezwa kimtindo,umenikumbusha chuo. mija umeshitukia barido imeanza kwa kasi,sasa kaka zenu wenye vimyama A.K.A ngiri kazikwelikweli yasinta unajuwa ugonjwa huo,wa mtu kupindwa na ngiri.kaka S

Yasinta Ngonyani 7:57 pm  

Sawa Mija nimekupata nadhani nilishamweka Maisha na Mafanikio akinengua..:-)

Kaka S. Nadhani haupo peke yako hizi blog za kiswahili zinasaidia sana.nanukuu "mija umeshitukia barido imeanza kwa kasi,sasa kaka zenu wenye vimyama A.K.A ngiri kazikwelikweli yasinta unajuwa ugonjwa huo,wa mtu kupindwa na ngiri.kaka S" mwisho wa nukuu! mmhh nisiseme umwongo sana lakini nadhani nimewahi kusikia sijui nisema hapa au? Ni hasa kwa kaka,babu au wazee kwa vijana kwa ujumla au?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP