Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kunawadaio UZURI ni BOMBA la NGAO ya WENYE TABIA mbaya kutostukiwa!

>> Tuesday, October 11, 2011

Ndio,...
.... yasemekana ili WATU waone MAKALI ya TABIA MBAYA za mwenye SURA NZURI,...
.... inabidi kwanza waruke SURA na UMBILE zuri la KIDOSHO ili wastukie anatabia mbaya au hata waanze kuingiwa WAZO kuwa labda PAMOJA na kuwa KIDOSHO  ni MREMBO kisura , tako , usafiri  pamoja na vikorokocho vingine vya kudakia WATOKWA UDENDA bado labda  anamchezo wakujikojolea KITANDANI bado mpaka ukubwani  na mara ya mwisho  KIDOSHO kujilowanisha akiwa  usingizini labda ni siku hiyohiyo aliyowekwa kwenye lensi  ya macho ya avutiwaye na sikioni  mwa aliyedakwa kwa sauti nzuri utafikiri ni ya malaika kiruka njia .

Swali:
  • AU? 
  • Na si kwa SILAHA ya UZURI yasemekana WAREMBO husamehewa UJINGA  kuliko siye wenye SURA mbaya?
  • SI unajua DUNIA yetu imejaa watu waaminio na kuthamini ya JUUJUU tu kitu kifanyacho kuwa kama YA MTU YALE MAZURI yamejificha chini ya LISURA lake baya kama ramani ya kipenyo kwenye tako la nguruwe, hayo yake mazuri anaweza mpaka kufariki hayajagunduliwa wala kustukiwa?

NDIO,...
... kuna wenye mambo BOMBA SANA  hapa DUNIANI  wakwepwawo na WATU  kisa tu KISURA imeaminika ni MAKATILI au tu sio watu wazuri.

Swali:
  • Si inasemekana kuna wadaio wapo watu WAZURI tu wenye tabia za KIMALAIKA waliokaa KIVIBAKA kitu kifanyacho wakisogelea tu WATU, mtuz huanza kujipapasa kama bado POCHI wanalo kwa kuamini KISURA tu wanajua KIBAKA ni nani?
  • Na sinasikia hata KIKUKOPA MTU kuna ambao kisura tu kuna wawakopeshao kisa wamekaa kama vile ngawira pesa wanazo kitu ambacho ni moja ya siri zao kwanini KITAPELI wao ni washindi?
  • Na si inasemekana kuna WAJUAO na ni muonekano wao tu hufanyao HAWASIKILIZWI  hata wakati wanatoa suluhisho?
  • Na siinasemekana kuna waliompigia mpaka Rais Kikwete kura kisa wanampenda SURA?

Ndio,...
.... labda SHETANI hajakaa kishetani afikiriwavyo,....
.... na labda ukitaka kustukia kuna uwezekano hapo au katika hilo yupo SHETANI,...
.... moja ya kitoacho siri ni kama hapo ni PATAMU kunoga na unajisikia vizuri sana hapo au katika hilo hata kama ni la KIZINZI  unajiaminisha  kuwa hilo ni KITENDO TU CHA NDOA na unogewavyo sio KIZINZI.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu Checo Acosta waingilie ghafla na kubadili mchezo kwa-La Cinturita




Choubou alainishe kidogo kwa-Andrea



Halafu WANAUME waturudishe tu tena- DAR mpaka MORO




Halafu T Pain azime kwa-5 O'Clock


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP