Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati kuna ambao KUTESTI ZALI kabla ya NDOA ili kucheki kama MIMBA inashika ni OYEEE kisana tu yani!

>> Saturday, October 08, 2011

Yasemekana  SIKU HIZI  ni UJANJA  kabla KIDUME hajaoa,...

.... kutesti zali KWANZA!:-(

Swali:
  • AU?

  • Lakini ,....JE ?
....kwani ni mangapi  inabidi tuamini  tu bila kutesti zali?
.... tunakoenda si itafikia WATOTO WA MAMAM KISEBENGO KILA MAHALI  kila wakati kutaka kucheki kuwa lile liaminikalo kuwa -NI siri ya MAMA KISEBENGO KIUHAKIKA ndiye ajuaye nani hasa  ni baba ya  MIMBA ya MAMA KISEBENGO  labda aijuaye si MAMA KISEBENGO pekee kwa UHAKIKA  kwa kutesti kuwa kitu cha kawaida katika DUNIA HII ambayo hakuna IMANI tena?

Ndio kunatuyajuayo yale ya UKIGUSA MOTO utaungua LAKINI ,...
.... na labda haihitaji  mtu mwenyewe KUTESTI zali kama umeona tayari  jinsi  mwingine  alivyogusa moto akaungua.


Swali :
  • AU?


Ndio,...
..... na labda kuna ambao  hata kwenda MBINGUNI  wangetaka kutesti ZALI kwanza ,...
... ili kucheki kama ni kweli kuna MBINGUNI kabla ya kuamini DINI zao.

Swali:
  • Kwani huoni  jinsi IMANI  ilivyopungua DUNIANI kitu ambacho  labda kuna watakao UHAKIKA tu na kusahau utamu wa KUAMINI tu?


Ila kama WEWE ni miongoni mwa waaminio ni UJANJA kutesti zali kwanza  kabla hujachukua JUMLAJUMLA,....
.... kumbuka kuna ambao katika kutesti zali kwa nia ya kucheki kama MIMBA inashika kishughuli ambazo kwa kawaida hufanyika PEKUPEKU,...
....kuna waibukao na gono, kaswende na UKIMWI na wakati huo bado MIMBA haijashika pia!
Swali:
  • Unabisha?

Ndio,...
.... ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


Hebu tu tena Patricia Faria abadili wazo kwa kurudia tena-Fofoca Joaquina




Yuri da Cunha arudie-Homem é bom




Buju Banton aingilie kati nakubasili mchezo kwa-Love Me Browning




Buju Banton apitilize kidogo na kuharibu kwa - Over Di Dickie




Mad Cobra ajaribu kulainisha tena kwa kurudia -Flex



Halafu Ray Barretto arudishe tena ustaarabu kijiweni kwa-El Watusi




Halafu Willie ROSARIO azime kistaarabu pia kwa -WATUSI Boogaloo



5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:54 pm  

Kweli tuendeako sijui ni wapi na je kama mimba haikamati nani atamchukua huyo? na utajuaje kama ni kosa la mwanamke?

Simon Kitururu 5:01 pm  

@Yasinta: Si nasikia ilikuwa ni siri ya WANAWAKE akistukia DUME halizai kisiri kufanyia kazi ya kupewa mimba kisiri kwa nje mamamkwe akishirikishwa?

Halafu si nasikia WANAUME huwa hawanakasoro?:-(

Yasinta Ngonyani 6:34 pm  

Siri? wanaume hawana KASORO? wao wanaamini hivyo na kumsingizia mwanamke...

sam mbogo 6:41 pm  

Katika hoja hii,ya kuzaa ama kutokuzaa,huwa tuna bebeshana lawama sana,midume husingizia kuwa ni demu ndo hazai,na demu husema mumewangu twende tukapime tuone tatizo likowapi.sasa meni iksha ambiwa hvyo weee, mkwara kibao ,nk.Lakini muhimu nikuongea/kuzungumza wote kwa manafaa ya ndoa, naikitokea dume jongoo hapandi mtungi basi tafuteni njia nyingine najuwa zipo. Ila katesti kabla ya ndoa mimi naona haina maana,mimba ni mimba tu.kitaalam kucheki damu zenu kama zina patana na mna weza kupata watoto hiyo poa.ila inaumasana mkikosa mtoto namshukuru mungu.changa, moto wazo,mfano umehangaika mpaka mkapata mtoto,mfano wa kiume halafu baadaye akikuwa una gundua nishoga!! utafanyaje.mawazomengine bwana?.kaka S

Simon Kitururu 3:11 pm  

@Kapulya: :-(
@Kaka S: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP