Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAMA WA KICHINA AGOMA KULIPA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI KISA JUMAMOSI SIYO SIKU YA KAZI

>> Saturday, October 08, 2011

Mama wa Kichina akiwa amechachamaa na kuelekea katika Jengo la NMB Tawi la Mbalizi Road Mjini Mbeya kuomba msaada kwa mapolisi.
Moja ya watumishi wa kampuni ya AAICO ambayo ndiyo wamepewa dhamana ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari jijini mbeya akitoa mnyororo kulifunga gari ya wachina hao huku mama wa kichina akilia kwa hasira
Mama wa kichina akimtolea maneno makali binti Eliza mkusanya ushuru wa maegesho ya magari huku mchina huyo akiendelea kugoma kuwa hawezi lipa ushuru siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko siyo siku za kukusanya ushuru


Mume wa mama mama wa kichina akijaribu nae kuwaelewesha wakusanyaji waushuru wa maegesho yamagari kuwa wameshazoea hivyo kutolipa siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko


Picha zaidi ya tukio hili tembelea: www.mbeyayetu.blogspot.com


Nimetumiwa na:
Fredy Tony ICT wa MBEYA Yetu BLOG

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:56 pm  

Pole na wao!! kaaazi kwelikweli...

Simon Kitururu 5:02 pm  

Kaaazi kwelikweli Yasinta!

sam mbogo 7:04 pm  

Tatizo hapa ni utaratibu. sikuzote tanzania yetu mambo huwa hayawi bayana,hawasemi mambo mengi amba waweza kuta yapo kisheria kabisa watu hawajui. yawezekana hata kabango kanako ainisha mchakato mzima wa kulipia maegesho hakuna.kwa hiyo wajanja wana patiepo hapohapo. simon unajuwa taratibu huku kwetu uk mpaka jumamosi unalipa baadhi ya maeneo na imeandikwa. pole sana mchina .kaka s

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP