Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chama cha MAPINDUZI na MAJINA NUKSI!

>> Tuesday, April 12, 2011

Unajua kuna majina yenye NUKSI- alianza mdau kuongea.

Basi unajua kinachofanya TANZANIA bado mambo zake kama ni gari basi limepinduka hilo,....
... nikutokana na nchi tokea ipate tu uhuru kuongozwa na chama chenye jina nuksi lenye neno MAPINDUZI!-mdau akaendelea.

  • Kwani unafikiri neno mapinduzi kwenye jina chama cha MAPINDUZI  maana yake halisi ni nini?

  • Si unajua kama kitu unataka kisimame kisawasawa kimaendeleo  hakitakiwi KIPINDULIWE na una fikiri MAPINDUZI ya chama cha MAPINDUZI hayapindui NCHI? -jamaa akaendelee.


Wakati nataka kuingilia hoja ,...
.... MDAU akaanza tena kuwa:
...kumbuka kama unataka kumtafutia nuksi hata mtoto wako wa kumzaa mwenyewe, basi mpe jina hovyo la kinuksi nuksi vile uone.

Ukimuita huyo mtoto wako TAABU usishangae maishani mwake akiwa na MISHIDA mitupu.


Ingawa najua kuwa neno MAPINDUZI kwenye jina Chama cha Mapinduzi halikuwa na maana ya MDAU  labda ,...
.... ila MDAU kafanya nitafakari majina ya VITU leo:-(


Naendelea KUWAZA!:-(

Na hebu Kelis akiwa na Too SHORT wabadili wazo kwa-Bossy


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP