Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika MAHANGAIKO ya DUNIA,....

>> Thursday, April 14, 2011

..... watu HUHANGAIKIA kitu!

Tatizo ni kwamba,.....
...VIHANGAIKIWAVYO vitu,....
.... sio vyote ni kweli vyastahili KUHANGAIKIWA!:-(

Swali:
  • SI vingi watu wahangaikiavyo kupata ni vya muda tu ?
  • Na si vingi watu wahangaikiavyo kupata wakisha vipata hustukia havina mpango?


Ndio,....
.....kuna mpaka waachanao baada ya kuhangaikia NDOA,...
..... mara baada ya kupitia kuhangaikia KUOANA na ndipo kitu kustukia!

Swali:
  • Unauhakika hata uhangaikiacho kusomea/KUJIFUNZA kina mpango maishani mwako?


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu tugewe steel pan na Sound Setters katika - It's Showtime




Silver Stars wagusie nao - It's Showtime



Au tu na Invaders warudie pia - Doh Be On Dat


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Rachel Siwa 6:27 pm  

Binamu kila siku tunahangaikia vitu,leo tukihangaikia ndoa baada ya ndoa watoto,ikiwa chakula baadae maji,ikiwa nyumba baadae shamba......

Nafikiri ndiyo mtindo wenyewe wa maisha @kaka Kitururu au.....nimejaribu kuwaza.

Goodman Manyanya Phiri 10:56 pm  

Mkuu, umegusa suala muhimu sana hapo: "tamaa"

Ninaweza nikawa nayo pesa ya kutosha kununua gari aina ya Rolls Royce. Lakini kama mimi ni mwalimu wa shule ya Shaaban Robert Dar es Salaam na naishi Manzese haina haja ninunue gari. Bora zaidi niendelee kupanda daladala. Lakini kwa tamaa na maringo nitanunua tu!


Kwa Kiingereza zipo "NEEDS" halafu "WANTS". (IN OTHER WORDS, YOU MAY WANT A ROLLS ROYCE, BUT YOU DO NOT NEED IT IF YOU ARE A NON-MAGNATE WHO LIVES A STONE'S THROW FROM HIS/HER OFFICE).

Siri ya mafanikio maishani ni kuweza kutofautisha: "WANTS" ni za kifahari?? (LUXURY) lakini "NEEDS" ni lazima upate kwa mfano: chakula.


Nafikiri Kiswahili chake ni maneno mawili na vile mtu anavyoweza kutofautisha:

1. "mahitaji"

2. "matakwa".

Simon Kitururu 7:22 pm  

@Rachel:Kweli kabisa ndio Maisha yenyewe hayo!:-(

@Mkuu Goodman:Nanukuu``Siri ya mafanikio maishani ni kuweza kutofautisha: "WANTS" ni za kifahari?? (LUXURY) lakini "NEEDS" ni lazima upate kwa mfano: chakula.´´. Yani umemaliza hapo Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP