Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Watu hudakwa na MAPENZI YA KITU na IMANI YA KITU kitofauti kama utachunguza katika vitu hivyo viwili wanatumiaje AKILI!:-(

>> Wednesday, April 06, 2011

Na  IMANI na MAPENZI,....

.... labda ni MUHIMU tu kwa WATU kwa kuwa mambo hayo yanaonjesha WATU,...
..... yale ambayo watu KIUHAKIKA hawataweza kwa uhakika kufikia KUYAJUA,...
... na ni kama tu dirisha tu  la WATU kuchungulia ni nini katika MAISHA YA MTU ambalo kwa kutumia AKILI  halitawezekana kwa uhakika kwa BINADAMU kujulikana.
Swali:
  • SI unajua katika maswala ya IMANI na MAPENZI  hakuna  PROFESA katika hayo  aliyekubuhu kuyajua mpaka mitazamoyake ndio iwe kwa uhakika ndio UKWELI mtupu?
  • Na si unajua kama katika MAPENZI yako unapiga sana makalukulesheni na fulu kutumia MIAKILI kama tu katika IMANI yako unanyambulisha sana KIAKILi na hauingii kichwakichwa bila tafakari kubwa  ya kuwa IMANI yako inaleta maana au la- Labda MAPENZI na IMANI yako  ni dhaifu aka NDOGO na fulu kujilazimisha?


Na labda,.....

ukikutana na adaiye anaelewa A mpaka Z za IMANI au MAPENZI,...
.... ni MUONGO huyo!:-(


Na hili ni wazo tu MHESHIMIWA!:-(


Hebu Rais mtarajiwa wa HAITI  MICHEL ´´sweet micky´´Martelly adinye - San Ou

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:06 pm  

Nimelipenda wazo la leo umelineno kwa ukweli na wala halijapinda:-)

Swahili na Waswahili 3:36 am  

hahaaaha @kaka Kitururu umewaza sana!lakini kaka eti wanasema mapenzi ni upofu hii imekaaje?

au maneno ya wahenga tuu!!!

SIMON KITURURU 8:41 am  

@Yasinta: :-)

@Rachel:Mimi nafikiri LUGHA zetu huwa hazina maneno ya kutosha kukabiliana na kuelezea yamkutayo MWANADAMU.

Kwa hiyo ndio maana unakuta watu kutumia neno MAPENZI ni kigugumizi. Mapenzi ni UPOFU, Mapenzi ni KIKOOZI na mengi kama hayo yote ikiwa ni jitihada tu za kujaribu kuelezea hali ambayo lugha ya kawaida inashindwa kudaka hali yenyewe.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP