Bado ukweli uko pale pale kuwa SIGARA , bangi, kidude, mbirimbi , POMBE mpaka NYANYA zilizokolezwa madawa ya kuua wadudu LABDA si nzuri kwa AFYA yako!:-(
>> Saturday, April 02, 2011
CHA kusikitisha ni kwamba,....
.... labda karibu kila kitu si kizuri kwa afya yako,....
.... ukitazama maswala kwa kuzingatia kuwa ,....
.... karibu MAZAO yote sehemu nyingi kutokana na madawa na mambolea yachumvichumvi NA MADUDE MENGINE yatumikayo ,...... tukiachilia jinsi WATAALAMU WA SAYANSI tuwaaminio kuliko WAGANGA WA KIENYEJI wazidivyo kuchezea mazao kwa KUYAKOROFISHA KIJENETIKS aka Ki- genetic modification ukiyachunguza,...
... labda hakuna lililosalama kihivyo hata kama unatumia kondomu.:-(
Kwa hiyo labda wakati unanyooshea watu kidole,....
... kumbuka LABDA ufanyacho kinamadhara yaleyele.:-(
Swali:
- SI kuchambia maji labda kuna madhara yaleyale ya kuchambia TISHU ingawa mchambia mchanga labda ndiye aonaye tofauti?
- Unafikiri afanyaye kitu makusudi huku akijua madhara yake na afanyaye bila kujua kama akimbiliaye KULA kula mboga za majani ambazo HAJUI tu kuwa zimekolezwa madawa GANI kisawasawa YAFANYAYE mtoto mzuri wakike awe TASA kama tu RIJALI awe na udhaifu wa KUDINDISHA MTALIMBO na ni afadhali tu angejilia NGURUWE ki nyama ya kitimoto- nani ni anaafadhali?
Hebu Carlos Santana arudie - Oye Como Va
Au tu Carlos Santana aje na Rob Thomas warudie - Smooth
13 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh!!!
Labda ni MADAWA YA KUUA WADUDU ndiyo yanayokufanya uwaze uwazayo na kutuwazisha vema ufanyavyo.
Labda dawa za kuua "vidudu" zimetusaidia.
Labda .......
Lakini sasa huyo nguruwe anakula chakula gani?
@Rasta Mubelwa: DUH!
@Mtoto Mzuri Yasinta:Kwani Nyuki anakula nini ambaye hafugwi na WATU?:-(
Mt. Nyuki anakula unga unga wa maua na miti.Lakini nguruwe anahitaji kulishwa na vyakula vingi alavyo nguruwe ndivyo tulavyo sisi wanadamu. ....nijuavyo mimi
@Yasinta: Sasa mbona uliniuliza kama una majibu?:-(
Ila unauhakika Adamu na Eva walikuwa wanafuga nguruwe au tuamini tu kuwa Nguruwe wanahitaji BINADAMu wawalishe na wakijitegemea watajipikilisha na UGALi itakuwa chakula chao?
Usikonde Yasinta! Nimepata hoja yako na kumbuka asili ya nilichokuwa naongea kwenye TARALILA ni MAWAZO tu!:-(
Na katika kuwaza kwangu bado naamini kuwa kuna wanyosheao vidole watu wengine kuwa wafanyayo si AFYA wakati hao wenyewe wafanyayo hayana AFYA!:
Ni hilo tu!
Tabasamu basi Kipenzi!:-(
Teh!Nimeipenda ya Adam na Eva...nafikiri kulikuwa na "nguruwe pori", hawa hawalishwi wanajilisha wenyewe, nawaza tu Mt.
Sasa kama hao nguruwe wanajilisha/walijilisha basi watakuwa nao wanakula wanakula chakula kilichopuliziwa madawa pia.. kutabasamu ha ha ha haaa:-(
@Yasinta: Mmmmh!
Kwahiyo unataka kusema Mchicha wenye MADAWA na NGURUE aaliyekula mchicha wenye madawa ngoma DROO ki kusaidia watu wajisikie kufakufa?
@Mwanasosholojia:
:-)
nanukuu "Swali:
SI kuchambia maji labda kuna madhara yaleyale ya kuchambia TISHU ingawa mchambia mchanga labda ndiye aonaye tofauti?
Unafikiri afanyaye kitu makusudi huku akijua madhara yake na afanyaye bila kujua kama akimbiliaye KULA kula mboga za majani ambazo HAJUI tu kuwa zimekolezwa madawa GANI kisawasawa YAFANYAYE mtoto mzuri wakike awe TASA kama tu RIJALI awe na udhaifu wa KUDINDISHA MTALIMBO na ni afadhali tu angejilia NGURUWE ki nyama ya kitimoto- nani ni anaafadhali?" mwisho wa kunukuu kwa hiyo labda tuaache kula vyote...najiuliza tu kwa sauti
@Mtoto Mzuri Yasinta: Mmmmmh!
Nini tena mbona mmmmmhhhh kwanini Mtakatifu wewe? Ningekuwa na .... we acha tu....
@Mtoto Mzuri mwenye macho ya GOLOLI Yasinta: MmmmH ! ,....
.....ilikuwa ni mguno tu wa kuashiria umenifikirisha!:-(
SI unajua Mguno MmmmmmH!,...
...dhambi zake ikiwemo kukubali , KUSIKIA utamu, ....nk?
ok! kumbe:-(
Post a Comment