Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Inasemekana SULUHISHO la mimba LABDA lipo tu kabla mtu HAJAPATA mimba!

>> Friday, April 15, 2011

Kwa hiyo labda,...

.....SULUHISHO lilikuwepo kabla ya TATIZO katika MENGI,.....
.... na kidhaniwacho ni TATIZO ni kizibua kishimo cha SULUHISHO ambacho hakistukiwi na wengi kabla ya TATIZO,.....
..... hata kama tatizo tuongelealo sio mtu kupata MIMBA!

Swali:
  • Si inawezekana MAGIMBI yalikuwepo tu na  NJAA kama tatizo ndio chanzo chakuzibua uwezekano wa BINADAMU kustukia MAGIMBI ni CHAKULA?


Ndio,...
..... kisuluhisho mpaka la ni wapi panafaa kwendea haja kubwa,
... labda CHOO ni popote ,...
.... ingawa ni mpaka MTU apate tatizo la kubanwa kisawasawa hadharani ,...
.... ndio anaweza kustukia urahisi wa jinsi atakavyofunuliwa njia na mahali hata kama ni nyuma ya BASI tu pale stendi,....
... kuwa SULUHISHO lilikuwepo  kabla ya TATIZO.:-(


Ndio,....
... labda suluhisho la kitu chochote kile ,...
....lipo kabla ya TATIZO na ukibinywa kisawasawa utastukia hata ukuta unafaa kuchambia!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na RUKSA kutolielewa!
Ijumaa na WIKIENDI njema!







Moja kwa moja hebu Saul Williams aanzishe kwa - Gypsy Girl




Saul WIlliams arudie tu kwa -Black Stacy




Saul Williams ajaribu kumalizia kwa ku - Talk to Strangers


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:18 pm  

"Inasemekana SULUHISHO la mimba LABDA lipo tu kabla mtu HAJAPATA mimba!" mwisho wa kunukua inawezekana kweli?..nawaza tu kwa sauti hapa ...labda katika kufikiria kuwa nitakuwa na mimba au ...mmhh naacha... nimeipenda hiyo picha yako ya kuchora:-) Ijumaa njema Mtakatifu!!

Simon Kitururu 7:20 pm  

@Yasinta: Ijumaa njema kwako pia!

Yasinta Ngonyani 7:54 pm  

Ahsante Simon na kumbuka UGIMBI KIDUCHU:-(

chib 10:45 pm  

Yaani Da Yasinta, bora usimwambie kiduchu, maana atakuwa anaongeza moja akisema one for the road in honour of Yasinta, na unajua roads za kutoka kwenye ugimbi hadi nyumbani kwake, nasikia kuna roads kama 9 hivi, sasa kila moja in your honour, wajua zitatimia ngapi?
Mt. weekend njema

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP