Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUJIOONA SURA kwa MREMBO kabla ya KIOO na PICHA kulikuwa kugumu kuliko MREMBO kujiona PAJA!:-(

>> Thursday, April 07, 2011

BINADAMU  wa siku hizi wamejiona mara nyingi kwenye VIOO na PICHA zao,....

.... kiasi kwamba hata wakifumba macho wanafikiri kuwa wana -AIDIA ya  wanavyoonekana na watu wengine  KISURA.:-(


Swali:
  • AU?

Lakini kwa kuwa MARA nyingine NI MTU MWINGINE  ambaye hustua mtu  kuhusu BONGE la CHUNUSI alilonalo,...
....au tu  hata kuhusu BONGE la UDENDA uliokauka pembeni ya bonge la DOMO baada ya kuamka uliovuja wakati muungwana kalala  ,....
..... tunaweza kuwa na AIDIA pia ya uwezekano  kuwa SI  kweli kila wakati MTU anajua navyoonekana,...
.... na hii ni HATA baada ya kuwa SIKU HIZI DUNIANI tuna VIOO vya kujiangalia na KAMERA ambazo zaweza kututonya MUONEKANO.:-(


Swali:
  • AU?

Ndio,...
.... kujiona ilikuwa LAKSHARI kabla ya KIOO na PICHA,....
.... na kama ulizaliwa ,....
....UKAKUA mpaka kufikia UZEE bila kujiona kwenye KIOO au kuona PICHA YAKO kama ilivyokuwa ENZI ZA MABABU,.....
.... ukionyeshwa PICHA ZAKO za UTOTO  kwa mara ya kwanza UZEENI ,...
... unaweza usijistukie kuwa kwenye hizo PICHA huyo ni WEWE!:-(

Swali:
  • Unafikiri kama wewe tayari ni KUBWA zima ungeweza kujitambua katika picha zako za utotoni kama  tokea utotoni hukuwahi kujiona kwenye KIOO au PICHANI?

  • Kwani unafikiri NI WAKUBWA wangapi katika picha wanafanana nawalivyokuwa WATOTO hata kama hapa hatuzungumzii ukubwa wa makalio?


  • Na umestukia kuna MITOTO jichoni mwa MASHUGA MAMA ni mpaka iwemikubwa ndio INAVUTIA kwa kuwa kunakitu imebadilika?

  • Na umestukia kuwa kuna MIZEE  KIBOGOYO siku hizi ambayo ukiona picha zao za zamani  kuna watakao tafsiri kuwa ilikuwa MIHENDISAMU aka inafaa kwa uasherati  wa burudani hasa kama nia KWA KIBONGE sio kuzalishwa watoto?

Ndio,...
....watu HUJIFUNZA  wanavyoonekana  na kufikia kufikiri wanajua wanavyoonekana  kitu ambacho labda SIO KWELI ,...
....kisaidiwacho na  VIOO na KAMERA siku hizi.
Swali:
  • Si unakumbuka uwezekano wa kuwa  hata KIAKILI labda KUBWA ZIMA halifanani na hilo kubwa zima enzi ya wakati bado TOTO?
  • SI kunauwezekano MTU ajionavyo ni tofauti na WATU wamuonavyo ikiwa AJIONAVYO na WAMUONAVYO wengine yote ni matokeo ya kujifunza jinsi ya KUONA kitu  -kitu kifanyacho kizuri kwako labda sio kizuri kwangu?


Ndio,....
.... labda bado ukweli uko palepale kuwa KILA siku  muonekano wa MTU hubadilika,....
... na ulivyokuwa unaonekana jana sio sawa na leo kama utaangaliwa kwa DARUBINI,...
... kitu kifanyacho YULE  WEWE wa UTOTONI , ujanani na UZEENI kuonekana tofauti,....
... hasa kwa kuwa NI TOFAUTI,...
...hata kiakili :-(


Swali:

  • AU?
Na ni  NDIO,....
... labda bado KUJIOONA  SURA  kwa MREMBO baada ya kugunduliwa  KIOO na KAMERA zitunguazo PICHA na zifanyazo MREMBO kujiona na KUJIKUMBUKA SURA kirahisi,...
.... hakubadili kuwa kwa MREMBO bado  kujiona SURA sio rahisi sana  kama kujiona chupi au PAJA:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu Ms Dynamite arudie tu - Dy-Na-Mi-TeeAu tu L. V. arudishe dubstep kwa - Turn Away

11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:54 am  

Nina wasiwasi kama ni Sura au Urembo ndio unaozungumziwa hapa au kitu kingine. kama ni hivyo basi najisikitikia sana maana sijawahi kuona sura yangu wakati nipo kachiki....

SIMON KITURURU 11:57 am  

@Yasinta: Ikitokea picha yako ukiwa ``KACHIKI´´ mmishenari fulani aliitungua na kamera lake la kikoloni enzi hizo na sasa hivi Bloga M3 kaitundika kwenye BLOGU yake ,...
... unafikiri utaweza kutambua kuwa ni PICHA yako?

Yasinta Ngonyani 1:09 pm  

Ndo hapo sasa sijui kama ntajitambua ni mimi lakini nahisi sikuwa tofauti na sasa au lazima kitu fulani kitasema ni mimi:-(

Malkiory Matiya 1:13 pm  

Siku hizi utaamba mwanamke urembo babu! Nimejifunza mengi kutokana na make up za akina dada wa kisasa.

Binafsi ningekuwa nachagua mke leo,ningeenda kutafuta kwa Wabarbaiq, hawa ni natural kama walivyoumbwa!

Yasinta Ngonyani 2:03 pm  

Kaka Malkiory nakuunga mkono haya ma-make up ningekuwa na uwezo ningebomoa maduka yote yauzayo hayo makolopwezo. Yanaharibu kabisa sura zetu.. huko kwa Wabarbaiq ni wanawake tu ndio natural au wanaume pia?:-)

Malkiory Matiya 4:44 pm  

Wanaume vazi lao ni mgorori na wanawake wanava marinda ya ngozi hakuna cha nguo ya ndani wala nini! mafuta ya kujipaka ni samli.Kwahiyo unaweza kujionea mwenyewe jinsi wanavyojali asili yao.

Mcharia 5:52 pm  

Nombeni Ramani ya huko kwa Wabarbaig tafadhali. Dha!! ila nimekumbuka kitu...ngoja kwanza.

Mcharia 5:59 pm  

Ni sawa na kumuona mtu anayejitapa kuwa yeye ni bingwa wa kuendesha magari na ameendesha meengi ya aina tofauti tofauti, suala likaja hivi; ilipoingia Automatic.

Kwa kuwa ni bingwa wa kuendesha magari watu wakampendekeza kuwa atafaa kuendesha na hili la Automatic japo ndio mara yake ya kwanza kusikia kuwa kuna gari yenye gia moja ya kuanzia nyingine zinajiingiza zenyewe kadri unavyokanyaga mafuta.

Yote ni kwamba si kila tuonacho ndio tuwe na hakika kuwa ndivyo kilivyo. Kuna aliesema mimi ni Handsome na kuna aliesema kuwa mimi huyu huyu ambaye nimeambiwa ni Handsome kuwa hata sivutii.

BADO INAFIKIRISHAEE

EDNA 7:03 pm  

Duuh,najaribu kuimagine hivi ingekuwaje kama kungekuwa hakuna kioo?
Mtakatifu SIMON umenifanya niwaze mbali sana.

Goodman Manyanya Phiri 10:50 pm  

Maisha ya kisasa ni haraka haraka. Unakwenda haraka haraka kwa wale wenye ufundi wa MAKE-UP...hasa ukiwa mwanamama... wakutengeneze haraka (au ujitengeneze mwenyewe kama unaweza).

Muda wa kujichunguza zaidi baada ya hapo huna, kwani uko bize kutafuta riziki yako ya siku.

Nisawa na mchezaji wampira anapopiga PENALTY. Kitaalamu ataangalia kwanza ziko wapi GOALPOSTS za wapinzani. Baada ya hapo macho anaangaza kwenye mpira tu, anaukimbilia na kuupiga ndani bila kuchunguza hata mara moja tena hizo GOALPOSTS kwakuamini hazijageuka wala hakujatokea mtetemeko wa ardhi kuziangusha!

Hiyo inaitwa SELF-CONFIDENCE siyo kila mara kujichunguza chunguza mara sura kwenye kioo tena mara viungo vingine mwlini wako vikoje tangu asubuhi...yanini, Mkuu?

SIMON KITURURU 12:03 pm  

@Da Yasinta: Lakini si kuna watu wazima wengi tu inasemekana hawafanani kisura na jinsi walivyokuwa watoto?
Kuhusu kubomoa maduka ya uzayo make up , utagombana weye na wanawake wenzako oooho!:-)

@MkuuM.W.M: Unaona sasa umemtia vishawishi kuhusu Wabarbaiq mkuu Mcharia,..
... shauri zako labda kashapata dhambi!:-)

@Mkuu Mcharia : SI utani inafikirisha aisee!:-(


@Edna: Vipi ungepata taabu ee kungekuwa hakuna kioo ee?Lakini usikonde kwa unavyovutia nafikiri kwa jinsi tu ambavyo sie midume tukuangaliavyo kwa uchu ungestukia tu unalipa mtu wangu!


@Mkuu Goodman:

Nakunukuu``Hiyo inaitwa SELF-CONFIDENCE siyo kila mara kujichunguza chunguza mara sura kwenye kioo tena mara viungo vingine mwlini wako vikoje tangu asubuhi...yanini, Mkuu?´´- mwisho wa nukuu.

Laiti kila mtu angekuwa anajiuliza hivyo na kuwaza kama uwazavyo MKUU!

Lakini ukweli ni kwamba SELF CONFIDENCE na vikorombwezo vingine vihusianavyo na kitu hicho NAHISI ni adimu aisee!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP