Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LUGHA haina MANENO ya kutosha hata ya KUTUKANIA tako vizuri , achilia mbali KUMSIFIA msenge!

>> Friday, April 08, 2011

Lakini kwa kuwa hata bila maneno YAKUTOSHA ,...
... atukanaye bado hufanikisha PIA kufikisha ujumbe kuwa katukanwa MTU,...


.... labda mahitaji ya MANENO ZAIDI ,...
....mpaka  ili kuelewa WENGINE TUTUMIE KAMUSI  ili tuelewe zaidi  kwa kinagaunaga ni nini anamaanisha kwa kusema ``ANAKUPENDA SANA kama NYAMA YA KUKU ´´ au tu  ILI  yule ajaribuye kutofautisha utamu wa ASALI na ule wa SUKARI kwa  MANENO hasa  kwa ambao hawajawahi kuonja ``SUKARI na ASALI´´,...
.... siyo ya MUHIMU SANA  kwa kuwa atukanaywe NYOKO hata bila kuelewa NYOKO ni nini kinamna labda hupata ujumbe auimajinio mwenyewe na ndio maana anakasirika.:-(

Swali:
  • Si unajua hasa kwa KISWAHILI kuna mpaka wanyama waishio TANZANIA ambao hawana majina ya KISWAHILI kwa kuwa maneno ya KISWAHILI hayatoshi?

  • Kwani hujawahi kushindwa kujielezea kisa hupati neno la kitu?

  • Na labda si  ndio MAANA WAZUNGUMZAO Kiingereza wanatumia maneno ya KILATINI katika baolojia kujaribu kujazia MANENO ingawa labda  MANENO saa nyingine wingi wake ni kwa ajili ya kujazia visivyohitaji kujaziwa na ndio maana katika kujazia maneno mpaka JIJI  kubwa kuliko yote TANZANIA lina jina KINENO  la KIARABU  ambalo ni Dar-es Salaam ingawa ki NENO  jina la asili ya KIAFRIKA la jiji hilo tokea  bado ni KAMJI lilikuwanalo na lajulikana?

Lugha haina MANENO ya KUTOSHA,....
.... LABDA ndio maana nashindwa kumsifu MPENZI kamaastahilivyo SIFA.

LUGHA haina MANENO ya kutosha,....
... na LABDA ndio maana hata MATUSI  kiufundi KWA WATU WENGINE ni vigumu KUYANOGESHA  kisifa mpaka yaweni MATUSI kisifa.
Na lugha  labda haina MANENO ya KUTOSHA,...
.... kwa kuwa  labda LUGHA hazihitaji kuwa na MANENO yakutosha hasa kwakuwa LUGHA kama watu tu ZINAZALIWA, na kufa kama tu BINADAMU na zinaubinadamu ambao hautosheki KISIFA.:-(


Swali:
  • AU?
Lakini ,...
.. LUGHA labda inatosha  kama ifanyacho ni NYONGEZA tu kwa mbayo hata bila maneno MAPYA tungepata kuelewa hata kwa kukonyezwa tu ni nini kinaendelea,...
....na kama MANENO mapya bila KAMUSI  yakiongezwa  hata yakitumiwa  alengwaye KWA NENO hawezi kuelewa!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


Sijui kwanini hebu
Amadou & Mariam waendeleze kwa - Je pense a toi



AMADOU & MIRIAM waendeleze zaidi kidogo kwa - Sarama



Halafu ilimchezo uishe Amadou &Miriam waje na K'naan katika- Africa


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 12:37 am  

Hongera na asante kwa kuleta hii hoja.
Nina swali sijalipatia jibu. Naamini nitapata ufumbuzi kwako.
Breakfast kwa kiswahili ni Kifungua kinywa, Desert ni kifunga mlo Je Starter na main dish zinaitwaje kwa kiswahili?

Christabell

Simon Kitururu 11:48 am  

@Christabell: Haki ya nani sina uhakika ,..
... ila nikibunia majina:
Starter naweza kuiita -Kilainisha Koo:-)
Main Dish nikaita-Chakula kikuu.

Ila hapo nimebunia tu kwa kuwa mie nilizoea kuitwa tu:
``Simon CHAKULA tayari!´´

Na ili kuwa fulu no kutofautisha majina kwa kiswahili .

Chai ni chai , NGUNA ni NGUNA , na aishikirimu ni aishikirimu.Na tukitembelewa na maforegner nyumbani . Lugha ilibadilika na mambo yote kugeuka kuwa ung'eng'e Breakfast, Starter, Main Dish , Desert .e.t.c :-(

Naombea kweli atokee kupitia hapa nguli wa lugha ya kiswahili kama Mkuu MATONDO atusaidie!


Profesa Matondo eeeh!
Msaada hapa basi Mkuu!

Anonymous 11:25 pm  

Asante sana Simon. samahani kwa kuchelewa kushukuru, ni kutokana na mihangaiko ya kidunia.
Nashukuru pia kwa kujaribu kujibu swali langu.
Matondo naona hajaitika.

Christabell

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP