Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STORI yangu, STORI YAKE na ukweli wenyewe IKIWA ni vitu VITATU tofauti!

>> Friday, April 01, 2011

STORI za GADDAFI stori za WAPINZANI wa GADDAFI na ukweli wenyewe LABDA ni vitu vitatu TOFAUTI!:-(

Washabiki wa OBAMA wamsifiavyo, WAPINZANI wa OBAMA wamkandiavyo na UKWELI wenyewe wa astahilivyo OBAMA kusifiwa labda ni vitu vitatu TOFAUTI.:-(

Wapinzani TANZANIA waongeayo, Washabiki wa CCM waongeayo na ukweli wenyewe labda ni VITU vitatu tofauti.

Swali:
  • AU?

Binadamu ni MPENDELEAJI,....
..... na kama unaangalia TAARIFA za HABARI au tu unamsikiliza MTU,...
.... kumbuka kuna uwezekano usikilizacho ni UPANDE mmoja tu wa HABARI na ukweli wenyewe LABDA  ni KITU tofauti.:-(
Swali:
  • SI unajua ni vigumu sana kwa WAZIRI MKUU wa UINGEREZA kumsifia GADDAFI hata kwa GADDAFI astahiliyo kusifiwa kwa kuwa habari kwa mtazamo wa KIMAGHARIBI kumsifia adui sio kitu kifagiliwacho?
  • Si unajua muwamba ngoma huvutia kwake?
Tatizo ni kwamba,...
...... kuna wadhaniao kwa kuwa KUNA upande una hoja nyingi za kutetea mitazamo yao ,...
... basi kwa hiyo huo UPANDE ndio uwakilishao UKWELI wa jambo kitu ambacho yawezekana sio KWELI.:-(

NI wazo tu!Hebu tusikilize kiletacho maana....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP