Hata kabla ya KUVAA TENA NGUO ukirudia kufikiria KILEKILE ulichowahi KUKIFIKIRIA mara ya KWANZA ulikielewa!
>> Friday, April 22, 2011
Unaweza kustukia KILEKILE kitu ULICHOFIKIRIA chochote kile mara ya kwanza ,...
....labda kina MAANA tofauti ukikifikiria TENA na TENA!:-(
Swali:
AU?
Ndio,...
.... labda chochote ukikifikiria sana ,...
...utastukia kina maana zaidi ya MOJA,...
... na ndio maana hakuna kitu kimoja kielewekacho kwa staili au TAFSIRI moja kwa kila MTU!:-(
Na kwa kuwa kitu kimoja kinaweza kuwa na MAANA nyingi,...
...... hata lugha utumiayo inaweza kuwa ndio ichangiayo UNACHOSEMA wakusikilizao wapate MAANA ambayo HUMAANISHI!:-(Ni wazo tu hili MKUU!:-(
Hebu Gyptian aingilie wazo akiwa na STEIN na kubadili kwa....
-Take You For A Ride
Au aendelee tu Gyptian kwa-Beautiful Lady
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Asante Mkuu!
Natahamaki kweli mawazo juu ya kitu chochote kile hayawezi "KUKAMILIKA". Nakumbuka hata MOVIE fulani ya Jackie Chan: mule mzee mzima anawauliza wageni mitaani ["NANI JINA LANGU?"]. Sasa wewe kweli mtu mzima itakuwaje usijuwe jina lako kikamilifu na maana yake kama wazo "LINAKAMILIKA"?.
Nakweli, yapo maneno kadhaa katika Kiswahili changu (Kizulu/Kiswati) nilietumia sahihi katika ka jamii yangu Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka 48 sasa lakini, hata kwa matumizi yangu sahihi, huwa nagundua mara hadi mara nilikuwa sijui maana ya maneno hayo kwa undani!
Inamaana ningekuwa chuo kikuu kwa ajili ya shahada kuhusu mameno hayo wala nisingefaulu!
Somo ninaejifunza leo ni hili: tuwe waangalifu sana tusije tukajigamba eti sisi ni wataalamu wa chochote kile duniani!
@Mkuu Goodman:Nilitamani kweli kuongezea kitu kirefu ,....
ILA umegusa kiini chandude kwa maoni yako haaaaasaaaa!
Mtakatifu,nimepata ujumbe.Naomba nitumie Ijumaa Kuu hii kuungama kuwa nimekuwa nikipita kiwanjani kimya kimya bila kuacha alama za unyayo...hahaha.Nimeanza rasmi kuacha alama.
Ijumaa Kuu njema Mtakatifu
@Mkuu Evarist: :-)
Ukweli hata mimi pale kwako mkimya kidogo! Ila nimefurahi sana kwa kuja kidogo kwangu kusalimia!
Si unajua sisi ni Majirani na NDUGU kwa hiyo labda kutengana isiwe kihivyo- kijumlajumla!
Pasaka njema Mkuu!
SHIKAMOO KAKA.
Post a Comment