Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa HAUSIGELI amezoea ladha ya MABOGA ,.....

>> Wednesday, April 13, 2011

.....kuna mama mwenye NYUMBA na mtoto wake WA kiume YULE aliyeanza kubalehe,.....
......watafikiri  HAUSIGELI anahitaji kufundishwa utamu wa KEKI!:-(



Kwa kuwa KUNAWAFIKIRIAO  ukizoea BOGA ,...
...KEKI ni JAMBO JIPYA;.......

....... na kama njemba imezoea utamu wa MABOGA, .....
.......ladha ya KEKI labda njemba inahitaji jinsi ya kuonja IJIFUNZE,....
....ndio totoz ZIJIFIKIRIAZO ni JANJA  zilivyofikiria!:-(





Swali:
  • SI WALI na UGALI wa mihogo INASEMEKANA vina ladha tofauti?

Ndio ,...
.... labda kama MAISHANI umezoea ladha ya KHADIJA,...
.....tabia hiyo  inawezekana kufanya  ZUBEDA awe sio mtamu kama unang'ang'ania awe mtamu kama KHADIJA!:-(


Na wazo hilo ,.....
... laweza kuwa  muanzilishi WAKE sio WEWE!:-(



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA  na labda wala kwa hili la kijinga usikonde!:-(

Hebu tu Mr Ebo arudie kitu classik kibongo fleva na kulainisha tena kwa -Mbado




Ngwair arudie classiki kibongo fleva ile-Mikasi



Au tu Mr Blue alainishe zaidi kwa klassiki ya kibongo fleva kwa kuongelea ya dogodogo saizi yangu  -Mapozi


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 12:17 am  

Ndio tuseme Mzee Gbagbo kwa kuzoea kwake sana keki akawa na mashaka kama ataliweza boga..

Kitururu haki ya nani ukizoea boga keki inakuwa ngumu kuizoea..

malkiory 12:45 am  

Mazoea yana taabu!

emu-three 8:24 am  

Mazoea kweli yana taabu, lakini wahenga wanasema `nyama zote ni sawa, hata kama mabucha ni tofauti...AU? TOFAUTI NI UPISHI TU!

Yasinta Ngonyani 11:11 am  

Mazoea hujenga tabia. Ukishazoea basi inakuwa hivyo:-(

Simon Kitururu 7:38 pm  

@Da mija na Mkuu Malkiory: SI ndio hapoo! Lakini mazoea yanazoeleka

@Mkuu M3:Mie nawasiwasi na utamu wa nyama kufanana lakini. Kwa kuwa nyama ya BATA na KUKU hasa kwa lugha ya pwani ni VITU TOFAUTI kwa kuwa kimoja chanuka mavi na kwa hiyo ni vigumu kuzifananisha.:-(

@Mrembo Yasinta:Ukishazoea unasahau vurugu zote za mwanzo zilianzia wapi. Nakumbuka nilipo kwenda Dodoma High School kwa mara ya kwanza mie na wadau tulikuwa tunamchezo wakununua maji ya chupa kisa hatutaki kunywa maji ya Dodoma kwa kuwa yanachumvi.

Nakuambia haikuchukua raundi tulipoanza kuchacha Maji ya chumvi yakageuka matamu na misosi ile mibaya ya shule ambayo tulikuwa tunairingia njaa ikiuma ilikuwa inakwenda kama kawaida kabisaa! Mpaka unajisahau ni nini ulikuwa unakiringia mwanzoni kujifanya nguna na maharage yaliyochemshwa bila mafuta wala kuungwa kuwa si matamu!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP