Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MONOGAMY aka siasa za mapenzi kiubahiri za CHANGU ni changu tu kama hicho KILICHO changu ni MPENZI WANGU!

>> Saturday, April 02, 2011

 Maswala ya :

  • Hivi ni kweli BINADAMU anatakiwa awe na Mpenzi mmoja tu?

.... yaliyosababishwa  na kamjadala  MTAANI nilikokuwa nagida MOJA moto moja BARIDI kabla ya kuelekea nyumbani LEO HII ulioletwa na ATIKO  ya Leanne Bell iongeleayo MONOGAMY ,...
.....  nakiri nimeyaachia katikati  YA MJADALA wakati  WADAU  wakiendelea kupambanua swala.

Paka nikimbie mjadala kutokana na MUDA na STIMU  vilevile ya KILAJI kuistukia inaanza kufanya ushirikiano wa miguu kuanza kuwa dhaifu  na kauli kistaili kuanza kugeuka  kimvuto na kunistua ninywacho ni POMBE na  sio CHAI  ,...
...mambo yalikuwa ngoma droo kati ya wale waaminio BINADAMU hakuumbwa awe na MKE au Mpenzi mmoja tu  na haya maswala ya MPENZI mmoja BINADAMU kajifunza juzijuzi tu na wale ambao wanadai BINADAMU sio MNYAMA na  kidude kimoja ndio astahilicho ,........ hapo mifano kibao iliingiziwa mpaka ya akina KING Solomon wapenzi wa MUNGU kuachiwa waoe mpaka wake Mia nane, King David mpaka kuua askari wake ili achukue mke  wa HUYO askari wake, mpaka tetesi kuwa kuna makabila ukichoma mkuki nje ya nyumba ya mtu  mke wake mali yako kwa hiyo siku ki kwenda mbele, BILA kusahau waaminio kuwa mazingira yakiruhusu kila mtu mpaka Papa Benedict anaweza kujikuta kafanya mashambulizi ya URODA kwa kuwa si kila siku binadamu ni SHUJAA wa kubania nanihiii........bila kusahau walioingizia maswala ya NI DHAMBI  kupewa tamutamu na zaidi ya mtu mmoja,...
.....na hata  UKIWA NA MTU MMOJA  ni mpaka MCHUNGAJI au SHEKHE aamrishe kuwa sasa kagidaneni.....


 ENIWEI,....

 Leanne Bell alichokoza mjadala HUU  kwa kuanza hivi ndude:

The same person...the same face, the same body, the same lips, the same everything, from this day forward for the rest of your life.

Can you handle it?

According to some people, it's like hell on earth.


Endelea HUKU

....kwa Leanne Bell
....http://www.andtheylivedhappilyeverafter.comSwali:
  • Wewe unafikiriaje? 
  • Kidude kimoja hata kama ni ANDAZI  chakutosha kiasi  kwamba Mkate , KEKI na vitumbua NO matamanio angalau ki ktutaka KUONJA tu?


Mie naendelea KUWAZA! :-(
Nisikudanganye ! Mie naenda zangu kulala ingawa ni saa sita tu na dakika sita usiku kitu ambacho ni mapema sana kwangu kwa kawaida kwenda KUMBONJI!:-(
JUMAMOSI njema MHESHIMIWA!

Hebu  Angélique Kidjo ambaye nimekuwa namsikiliza tokea niingie homu aje na Carlos Santana waanzishe upya kwa - AdoumaAu hebu Angelique Kidjo aongezee dozi kwa -BabalaoAngelique Kidjo adinye-WEWEAu amalizie tu kwa -Agolo


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:43 am  

...mbona naambiwa kama kila mtu atakuwa na mpenzi mmoja tu maishani basi kuna wanawake lukuki watakosa wapenzi eti kwa kuwa wao wapo wengi sana.......

SIMON KITURURU 2:44 pm  

@Mkuu Fadhy: Ndude hiyo na mimi nimewahi kusikia!:-(

Cha kujiuliza ni kuwa :
SI nasikia sikuhizi kwa MADEMu ujanja ni kuwa WASAGAJI?
Na kwani ni lazima kila mtu awe na Mpenzi?:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP