Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Msauzi GOODMAN MANYANYA PHIRI wa kibongobongo!

>> Monday, April 25, 2011

Kuna baadhi ya watu wanafanya nijifunze sana vitu kirahisi VITU!


Huyu Mkuu GOODMAN MANYANYA PHIRI ambaye anatoka AFRIKA KUSINI kwa jinsi asapotivyo WATANZANIA na au tu aandikavyo KISWAHILI kitu ambacho kama usingejua ni MSAUZIAFRIKA labda ungefikiria ni MTANZANIA,...
.... mie kuna kitu hata kwa utu wake ananifurahisha nakunifunza!





Kama hujamstukia ,....
Ni huyu hapa KIMTANDAO


Nimewaza tu kwa SAUTI WAHESHIMIWA!:-(



Hebu Msauzi mwingine anizinguaye ambaye ni Hugh MASEKELA aanzishe vita mpya kwa ndude iliyotuna-Khawuleza





Aendeleze vita kwa -Thanayi



Au tu na Msauzi mwingine nimzimiaye Abdullah Ibrahim atekenye tu - Cape Town Flower



Au tu Abdullah Ibrahim amwage tu na rojorojo  - IshmaĆ«l


11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Rachel Siwa 12:23 pm  

kaka Simon hata mimi namkubali sana tena sana, Nafikiri ni upendo na kuthamini wengine imejaa ndani ya roho yake,Si mbaguzi na mwenye kupenda kazi na maisha ya wengine, mimi pia nimejifunza na kuendelea kujifunza kupitia kwake.

Hongera sana kaka GOODMAN MANYANYA!!MUNGU AKUBARIKI.

Simon Kitururu 12:27 pm  

@Rachel: Nashukuru kumbe siko mwenyewe katika hilo!

Na MUNGU ambariki huyu MKAKA ingawa nahisi kashabarikiwa ndio maana ni mtu Mzuri hivyo!:-(

Mwanasosholojia 12:43 pm  

Wakuu ni kweli, nilikuwa nafikiria kuandika kitu kuhusu huyu ndugu yetu Phiri, Mtakatifu umewaz kitakatifu ukanitangulia, Phiri anastaajabisha kidogo kutokana na haiba yake pamoja na kwamba sijawahi kuonana naye ana kwa ana, kusoma maandiko yake kunanisaidia kuona huyu ni mtu mwenye upekee wa aina gani

Simon Kitururu 12:47 pm  

@Mwanasosholojia: Kumbe nawe MKUU umestukia eeh hii ndude!

Yasinta Ngonyani 1:08 pm  

Nakubalina na waliotangulia na nakushukuru Kaka Simon kwa kuandika mada hii. Huu nao ni upendo na pia ni mtindo mzuri wa kupeana moyo au nisema feed back...Hongera sana kaka Goodman:-)

Simon Kitururu 1:13 pm  

@Yasinta: Kumbe umestukia nawe eeeh!

Unknown 1:19 pm  

Kwanza ana mke na watoto wa 3, Daktari wa vita mzee.

NANUKUU BAADHI YA MANENO/MACHAPISHO YAKE: Siku za kuzaliwa, kama mwaka mwisho, inaweza kuwa kwa baadhi ya vyanzo vya furaha kuu wakati kwa wengine ni majanga hasa kwa wale ambao kihisia si juu ya jinsi matendo yao yalivyo. MWISHO WA KUNUKUU.

Jamaaa DUH. Kama vipi ahamie BONGO YANI.

Rachel Siwa 1:21 pm  

Nikweli kaka Kitururu amembariki!!!!!

Mzee wa Changamoto 1:36 pm  

Nimewahiwa

malkiory 4:21 pm  

Manyanya Firi, amesomea Tanzania na kuishi japo si kwa muda mrefu na pia moja wa wake zake ni mtanzania. Kinachonivutia ni mapenzi yake na uelewa wake wa Tanzania na jinsi anavyoimudu kiswahili pengine kunizidi mimi ambaye nimezaliwa na kuishi maisha yangu yote Tanzania. Ni jambo la kufurahisha sana, ninaimani Manyanya anao uraia wa pande mbili na kama hana basi tunamkaribisha kwa moyo wote Tanzania, kama atapenda kuja kuishi.

Simon Kitururu 4:28 pm  

Mmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP