WEE MTANZANIA labda SIMAMA na kusikiliza WIMBO wa TAIFA wa ZAMBIA kisaundi!
>> Thursday, April 28, 2011
Kuna haja ya AFRIKA kukumbuka kwanini NYIMBO hizi katika nchi kadhaa ukitoa maneno ZILIFANANA!
Haya wewe pale simama na sikiliza hili BITI toka ZAMBIA halafu wakati huohuo fananisha na wa BONGO kisaundi!
Endelea kusimama TWENDE Sauzi AFRIKA wakati umesimama na sikio lako linasikiliza BITI la wimbo,....
AU endelea KUSIMAMA tuusikilize tu na wa TANZANIA tena...
Kama hujastukia:
Madhumuni ya BARUA hii ni kuuliza:
- SI unajua wimbo wa TANZANIA haukutungwa na MTANZANIA?
- Au unafikiri ni MTANZANIA alitunga wimbo huu KI SAUNDI wakati nakuchokoza ujikumbushe jina lake ni nani?
- Na si unakumbuka ni KWANINI nchi kadhaa AFRIKA zilitumia BITI moja ingawa maneno tu ndio tofauti wakati AFRIKA tuna UMOJA enzi hizo?
Ndio,...
....inawezekana akina NYERERE, Kaunda na WENGINE walioanza kukubaliana MPAKA nyimbo za TAIFA zianze kufananafanana KUTOKANA na UMOJA labda walikuwa ,........ na BIG PICTURE kuhusu AFRIKA tuelekee wapi kiasi kwamba usipokuwa MFIKIRIAJI unaweza kusahau HILO siku hizi.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu tubadili wazo kwa kusikiliza wimbo wa ZIMBABWE ambao nahisi ukiondoa neno ZIMBABWE na kuweka TANZANIA laweza kufiti TAITI TU na kuendeleza MAANA ileile,....
.....na HEBU Henry Olonga mcheza KRIKETI maarufu duniani kutoka ZIMBABWE aimbe huu -OUR ZIMBABWE -na wakati wewe unausikiliza kwenye ZIMBABWE weka TANZANIA uone kama haufiti KIAINA hata kwa wale wadaio Tanzania hatujawahi kuwa na Segregation na kuita WAHINDI magabachori sio ubaguzi wa rangi:
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Wewe Simon unakazi kweli! Ebu nikuulize: kaenda wapi sasa Ndugu yangu Anoni mwenye kujitokeza kwa matusi ya "jalalani kwa Simon" hapo majuzi?
Kwa wasiejuwa nitawakumbusha ki hivi:
http://simon-kitururu.blogspot.com/view/flipcard/7475665297347333006/2011/04/kwani-mkundu-na-mdomo-kwa-binadamu-ni.html
ANYWAY, ubarikiwe sana, Simon. Wazazi wako walikutabiri kwa jina la "Simon".
Kama Simon Jabali (SIMON PETER "THE ROCK") katika maandishi matakatifu, mengi ya Kiafrika tutayasoma kwa kupitia blogu yako na mimi nakuhakikishia hukuokotwa jalalani kama mwenzetu alivyodai majuzi.
Chanzo cha nyimbo hizi za kitaifa kufanana ni lijamaa moja lenye jina la PIXLEY KA-ISAKA SEME (Yaani Pixley Mtoto wake Isaka Seme), Msauzi mwenye kabila la Watonga. Yeye Seme (http://en.wikipedia.org/wiki/Pixley_ka_Isaka_Seme)ndie mwanzilishi wa chama tawala Afrika Kusini. Pia yeye ndie aliyemlea kiakili mtu fulani anayejifanya leo ndiye mwanzilishi wa uhuru Afrika Kusini (mtu mwenyewe sasa anakandamiza jina la Seme kutokana na XENOPHOBIA nchini bondeni hapa kwani Watonga sio wengi Afrika Kusini kama huko Zambia, Mozambique, Malawi ETC).
Seme pia alikuwa ni mwanasheria maarufu.
Ndoto yake Seme ilikuwa sisi wote Waafrika tuwe nchi moja kama ndoto yake Shaka Zulu, mfalme wa kwanza waWazulu.
Bahati mbaya, Pixley Seme na Shaka Zulu wote waliandikiwa historia mbaya na Waingereza na sifa zao zikapewa wanafiki na wezi wengine wa kisiasa wanaojifanya leo ndio "Baba za taifa la Afrika Kusini" nayo ikiwa moja ya sababu za kusababisha chuki bondeni kwa Waafrika wasiekuwa wa makabila ya viongozi hao wanafiki.
Bahati mbaya sijausikia wimbo wa Zimbabwe; lakini ni sababu ya wanafiki wa huku bondeni waliosababisha Mjomba Bob kubadili wimbo wa taifa lake uwe tofauti, nahisi.
Kifupi, kwangu ni jambo la kujigamba kwamba wimbo waTanzania, Afrika Kusini, Zambia ETC. ni wimbo moja.
Tunataka tuvunje mipaka hii ya kipumbavu, na tutavunja tu... mipaka ya wakoloni inaofurahiwa na vibaraka vyao vya ukoloni wa mambo leo.
Kilipoanzishwa chama-tawala hapa kwetu, walialikwa viongozi wa Waafrika wa Afrika Ya Kusini kote na ndio maana tulianza kuimba wimbo moja.
Mwaka kesho, tarehe 8 Januari, Chama tawala Afrika Kusini aliyeanzisha Dr Pixley Seme kinamaliza miaka 100 lakini hakika huyo Mtonga (Seme), kama mwanzilishi huku wa vyama vya wafanyakazi aliyekuwa ni mwenyeji wa Tanzania/Malawi (Clemens Kadalie http://en.wikipedia.org/wiki/Clements_Kadalie)hatapewa sehemu yake ya heshima kwa kuwa Mwaafrika bado anakubali "historia yake ni ile aliyeandika adui yake Mkoloni wa Uingereza"!
@Mkuu Goodman:
PIXLEY KA-ISAKA SEME na ndoto yake: ``sisi wote Waafrika tuwe nchi moja kama ndoto yake Shaka Zulu, mfalme wa kwanza waWazulu.´´
Kwa bahati mbaya nahisi viongozi wetu wa AFRIKA wa siku hizi wameisahau!
Na kibaya zaidi historia za watoto wa Taifa la Kesho zinachakachuliwa na akina PIXLEY wanaachwa nje!
Yani mpaka kufanana kwa hizi nyimbo kumebakia tu kwa kuwa ni tamu masikioni lasivyo chanzo kilichosababisha kuwe na nyimbo zinazo fanana ambacho kilikuwa ni UMOJA wa AFRIKA kama ni mgonjwa basi yuko mahututi!:-(
Tatizo kubwa ni uchu wa madaraka ambao unasababisha baadhi ya mawazo na malengo mazuri kufifia au kufa kabisa.
Christabell
Post a Comment