Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mipaka ya BINADAMU,....

>> Friday, April 29, 2011

... kwa kawaida inawekwa na BINADAMU hasa atafsirivyo VITU.


Na mpaka hata wa NCHI waishizo BINADAMU,....
.... kama mipaka ya nini UKIVUKA hata KIFIKIRA unaonekana umevuka MPAKA,....
.... kwa kuwa inawekwa na BINADAMU,....
.... labda kwa BINADAMU hivyo sio vitu vya KUDUMU!:-(

Swali:
  • SI unaweza kukuta labda asilimia zote za MIPAKA uliyojiwekea MAISHANI hata ile ya kuhofia ukivuka hapo UTAVUNJA maadili ya JAMII labda kikweli ni WEWE mwenyewe UMEJIWEKEA na KUJIPIA hizo N'gwe?


Mipaka ya BINADAMU ,....
.... inapindika BIANDAMU wakitaka,....
.... inaongezeka kama tu WAKIMBIAJI waongezavyo rekodi kila siku ambazo huvunjwa,...
... lakini labda kikubwa labda MIPAKA ni  chazo cha kujinyima UHURU,....
.... na ukishakosa UHURU na UKAZOEA kutokuwa HURU  unaweza usielewe WAVUNJAO mipaka na kuwa HURU angalau hata kwa kusema wanachowaza bila kuhofia JIRANI na JAMII kwa ujumla itasema nini.


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu tu Herbie Hancock na Céu warudie - Tempo de Amor




Kama unataka kujua maneno ya wimbo kwa ung'eng'e ni:

Oh, it would be so much better to live in peace Without having to suffer Without having to cry Without having to want Without having to give yourself (2x) But you have to suffer and you have to cry and you have to want To be able to love Oh, deceiving world peace doesn't mean "love" anymore Oh, there is no sadder thing than to have peace and to regret and to submit and to protect yourself of a love, of loving

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 2:30 am  

Wengi wanaamini binadamu ndiye Mungu. Na kama akitaka kuweka mipaka ni haki yake!

Simon Kitururu 10:54 am  

@Mkuu Goodman: Tatizo Mipaka ya BINADAMU mara nyingi inaudhaifu wa huyohuyo BINADAMU hasa kwa kuwa anamchezo wakuamini anaposhindwa yeye basi Binadamu wengine nao mipaka yao iwe hapohapo!:-(

Unknown 2:00 pm  

Mipaka sio kwa binadamu tu, hata viumbe vya asili pia, ukitazama kwa kina utagundua jinsi kila jambo lilivyowekwa kwa usawa.

Ukiifikiria bahari nayo!! yaani jinsi kulivyo na mipaka majini na hata nchi kavu, labda niongezee kwa kauli kuwa:

Kuna mipaka kati ya waislam na wakristo katka kuamini kwao, matendo na mengineyo na inashangaza hata namna ya uelewa ilivyo.

Kama vile kulivyo na mipaka ya nchi na nchi, bara n.k ndivyo pia kulivyo na mipaka ya uvaaji kwa wanaume na wanawake.

Hata katika blog kuna mipaka.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP