Wakati tunakagua CHUPI ya MHESHIMIWA kwa JICHO !
>> Saturday, April 09, 2011
Katika UCHUNGUZI kiukaguzi,...
...labda chupi ya KITU ni rahisi kuchunguzwa,...
... hasa kwa kuwa kiuchunguzi SHATI au SKETI ya KITU hudhaniwa haihitaji sana UCHUNGUZI kiukaguzi hasa kwa kuwa inafikiriwa ni rahisi tu kwa jicho hata lenye kengeza KUANGALIWA!:-(Swali:
- AU?
Na ukaguzi wowote nia na MADHUMUNI yake ni ,...
... kwa MKAGUZI kustukia kitu,...
.... kiwe ni kile KISICHOSTAHILI kuwepo kwenye kitu ,...
..... au tu ni kiwe ni kile kidhaniwacho hustahili kuwepo hata kama ni DOA la haja ndogo kwenye kitu.:-(Swali:
- AU?
Na labda ukimwambia mtu akague SHATI CHAFU la mtu,...
....au akague CHUPI CHAFU ya mtu ,...
....maandalizi ya UKAGUZI yanaweza KISAIKOLOJIA kumuandalia MKAGUZI GLOVES aka kondomu za mikono/Mipira mfuko VIZURI -katika ukaguzi WA chupi chafu kidogo wakati akawa tayari kulishika SHATI CHAFU kuliko chupi kwamikono mitupu/bila gloves katika UKAGUZI - kwa kuwa TU LABDA shati CHAFU limezoeleka kuonwa ,.......na chupi chafu ya MHESHIMIWA ni nadra kuonekana na kwa hilo kuhusishwa na mengi yaoanishwayo tu na KAZI ZINUKAZO za matundu ya mwili yasitiriwayo na chupi ya MHESHIMIWA.:-(
Swali:
- AU?
Na MATOKEO ya UKAGUZI wowote wa KITU utumiao MACHO,...
..... labda unahitaji kwanza MKAGUZI kukaguliwa ayatumiayo katika UKAGUZI hayo MACHO.:-(
Na uzuri wa UKAGUZI wa CHUPI ya MHESHIMIWA kwa MACHO,...
....labda huwezeshwa haswa zaidi na uwezekano wa kuwa unaweza mpaka kumvua hiyo CHUPI mheshimiwa kitu kiwezeshacho urahisi zaidi wa KUIGEUZAGEUZA au tu hata KUIBENJUA ili ndani kuwe nje hata kama madhumuni sio kuinusa kidogo wakati umeileta hiyo chupi PANA karibu kabisa na MACHO.:-(Swali:
- Si unakumbuka lakini WATAALAMU wenye MACHO MAZURI TU bado ikibidi huhitaji DARUBINI kuona mengine hata kama hayo sio chupi na hayako kwenye chupi?
- SI kuna uwezekano kama MKAGUZI mwenye macho mabovu anaweza kufikia hitimisho chupi inadoa la mkojo kisa chupi ya MHESHIMIWA inanuka mkojo ingawa ni kweli kwa kutumia MACHO chupi hiyo haina hata doa moja la mkojo?
- Na si labda chupi inukayo mkojo katika uchunguzi wa pua sio lazima ilikojolewa kwa kuwa labda harufu ya mkojo ni kemikali tu ambazo labda ziko tu hata nje ya mkojo?
- Na si doa la NJANO likiwa kubwa sana na kukava chupi nzima ndio kitu kigeuzacho chupi nzima kuitwa ya rangi ya NJANO?
Katika uchunguzi wa MACHO,....
......ukubwa wa DOA huweza kuonwa kama ndio rangi ya KITU kwa kuwa rangi ya kitu labda ni DOA tu kubwa ambalo limetawanyika na kukava kitu kizima ,...
... na ukubwa wa kitu CHOCHOTE ukizidi labda pia hata uwezo wa kitu kuonwa kitu hupungua ,....
.... kama tu udogo wa kitu kama DOA upunguzavyo uonekano wa DOA kwa macho kwenye chupi au tu KITU kwa udogo wake tu .:-(Swali:
- AU?
Kwa hiyo,...
..... labda katika uchunguzi wowote ule kumbuka kuwa,.....
... labda UKUBWA wa kitu ,...
...kama TU udogo tu wa kitu ,...
.... vyote huweza kusababisha kwa kutumia JICHO usione kitu!:-(...kama TU udogo tu wa kitu ,...
Ni wazo tu HILI MKUU!:-(
Jumamosi na WIKIENDI njema!
Hebu twende Trinidad & Tobago ambako miziki NA wanamziki wake hunikuna tokea NILIVYOINTROJUZIWA na mpenzi kutoka huko -enzi za kuwa na mpenzi atokaye nchi hiyo ,...
.....HEBU tu Benjai aanzishe NDUDE kwa -Ah Trini..
Tubakie Trinidad & Tobago mwanamke nguli Ella Andall arudie kudinya-Black Woman
Ella Andall aingie ndani zaidi kidogo kwa-Bring Down The Power
AU tu tusogee tena pembeni kidogo ya T&T tukakutanishwe na Peter Tosh ili atoneshe tena kwa kurudia-Mama AFRICA
Nipo....:-(
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kaazi kwelikweli Jumamosi na wikiend njema nawe pia mt- Simon...
@Yasinta:Wikiendi njema kwako pia!
Post a Comment