Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Umuhimu wa UFUNGUO labda upo tu kama tu kuna MLANGO!

>> Tuesday, April 26, 2011

Na ufunguo ni UFUNGUO kama kunacho UNACHOFUNGUA,...

.... hasa kwa kuwa LABDA ufunguo ni kitu tu  uonacho jalalani kisicho na mpango ,....
.... kama hauna unacho FUNGUA!:-(
Swali:
  • SI ushastukia UFUNGUO na MLANGO ufunguliwao inatakiwa VISHABIHIANE ili UFUNGUO ufanyekazi zakufungua na kufunga?Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu SANCHEZ aingilie kati wazo kwa- Baby Can I Hold You TonightAu tu FOXY Brown abadili mchezo mzima kwa kurudia -Hot Spot


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:29 pm  

Mmmmmhh, kaaazi kwelikweli...

emu-three 2:00 pm  

Ufungu ...mkuu tungo tata hiyo!

Goodman Manyanya Phiri 5:45 pm  

Yale yenye thamani kuliko yote maishani ya binadamu, hayana ufunguo.

Mifano: mawazo, upendo, hewa, maji, ardhi.

Ukiwa daima umebeba ufunguo na unataka ukumbuke kila wakati ufunguo umeuweka wapi, wewe basi mtumwa wa mambo yasiekuwa na umuhimu kama maisha yako na binadamu wenzako!

SIMON KITURURU 2:14 pm  

@Yasinta+Mkuu M3: Mmmmh!

@Mkuu Goodman:Umenigusa sana na hii:


``Ukiwa daima umebeba ufunguo na unataka ukumbuke kila wakati ufunguo umeuweka wapi, wewe basi mtumwa wa mambo yasiekuwa na umuhimu kama maisha yako na binadamu wenzako!´´

Mcharia 1:21 pm  

Unapotukumbusha kuhusu ufunguo kumbuka pia kuna REMOTE kwa mujibu wa nyakati hizi za sayansi na teknolojia-kikarne.

Duh! ila huo ufunguo...mhu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP