Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwani MKUNDU na MDOMO kwa BINADAMU ni nini ni MUHIMU zaidi?

>> Saturday, April 23, 2011
Ndio,...
... kuna watumiao MDOMO  kula wasahauo kuwa ,...
.... kama MKUNDU haupo walichokila kwa MDOMO ni tatizo mwilini kama hakitatoka MWILINI!Swali:
  • AU?

Na kwa kuwa KIBINADAMU kuna wachaguao umuhimu wa VITU mara nyingine kwa kuwa,...
.... labda hawajavifikiria kiundani wavipavyo KIPAUMBELE kuwa labda havijitegemei kiumuhimu,....


.... ndio maana labda kuna wasifiao MDOMO ZAIDI bila hata kukumbuka kuwa kazi za MDOMO zinahitaji ujemadari wa MKUNDU pia ushughulikiao VINUKAVYO mwilini.:-(Swali:
  • Kwani unafikiri kwa BINADAMU ni KICHWA muhimu sana kuliko TUMBO au kikojoleo?
  • Kwani unafikiri KUKOHOA ni muhimu kuliko KUCHEUA?

Ndio,...
.... hata MAISHANI,...
...kinamna labda VYOTE ni MUHIMU aisee!


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na usikonde!:-(


Ngojea basi P Square na Bracket walainishe kwa-No TIME
 P Square warudie klasiki na J Martins ile ndude iliyotuna- E No EasyAu tu J Martins na Fally Ipupa watumbue tena jipu kwa-Jupka


14 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mwanasosholojia 4:08 pm  

Mtakatifu hili nalo neno..ni kweli tunakisahau kiungo hiki muhimu, teh!teh!

SIMON KITURURU 4:13 pm  

@Mathew Agripinus Senga: :-)

Mcharia 6:38 pm  

Myaaaaaayo!!! Duh.

Mwanasosholojia 8:51 pm  

Labda fadhila pekee huwa ni kukiosha/kukifuta tu eti kwa vile kimepakazwa uchafu uliopitia mdomoni:)sijui ni ujira au shukrani?nawaza tu kwa maandishi mkuu!

Swahili na Waswahili 9:09 pm  

Duhhhhhhh!hujambo lakini?

Goodman Manyanya Phiri 10:19 pm  

"Ni nini muhimu zaidi"?

Hamna kabisa!

Lakini hata hivyo kusema viko "sawa" nao usemi kama huo utakuwa si ukweli kwani huko bondeni hamna uwezo wa kupata ladha; hamna maombi kwa Mola; hamna uwezo wakumwambia wako "Nakupenda"; hamna namna ya kuomba msamaha; hamna vicheko; hamna maongezi; hamna ishara kwa daktari mwenzio amepata mafua; hamna uzuri wa kisura; hamna uwezo wakubadililisha OXYGEN kwa CARBON DIOXIDE; hamna uhuru wa kujenga wala kubomoa kama hivi kauli inavyoweza kufanya kutokana na mdomo; hamna muziki; na kadhalika.


Na ndiyo maana mimi, Mkuu Simon Kitururu, hua napata matitizo na wanablogu wanaodai kila kiungo cha mwili ni "sawa" na kingine; wale wanaodai vyote viwekwe hadharani na tusivae hata nguo kutokana na "ule usawa wa viungo" kwa kimawazo yao! "MECHANISTIC VIEWPOINT", kwa msemo wa Kizungu!

Lakini, si sote tunao uhuru wakuwaza kama tunavyopenda??? SO,I REST MY CASE!!

Anonymous 10:25 pm  

hivi wewe simon umeokotwa jalalani maana mambo yako yakijinga ya kitoto ya kipumbafu hukuwi wew ni mtu mzima jiheshimu na wewe utaheshimika sio kila siku tu uandike pumba hapa hata kama blog ni yako unajishusha hadhi sio ufahari na wala sio sifa kuandika matusi kama huna chakuandika funga blog sio lazima uandike watoto wako watajifunza nini kutoka kwako umemuona nani anandika ujinga kama wewe labda mvuta bangi au madawa y kulevya sura yako nzuri lakini kauli yako mbaya unayoandika hailingani kabisa na mwonekano wako hembu kuwa mstarabu bwana heshima hainunuliwi usiige mambo ya kigeni sisi wtz tunaheshima na tunadhamini tamaduni zetu

Goodman Manyanya Phiri 10:41 pm  

@Anonymous

Blogu sio kama gazeti la taifa au la chama chochote tawala pale duniani. Kila mmoja anao uhuru wa kuandika yake. Nawe kama wataka kuandika matakatifu, mazuri na masafi, basi fungua blogu yako na umwache Simon Kitururu aandike yake tafadhali!


Vilevile toka gizani la u-ANONYMOUS ila tujuwe wewe kabila gani.

Wadai kunamambo ya kigeni?? Kigeni gani wakati kila binadamu ni mtoto waMswahili?

SIMON KITURURU 12:09 am  

@Rasta Mcharia: :-)


@Mkuu Senga; Kuwaza saaa nyingine noma kweli yani!


@Rachel: SIjambo mtu wangu!

@Mkuu Goodman: Kuna watu ambao kuongea nao nivigumu.

Swali kwa waaminio kuna kitu spesho:

Lakini, si sote tunao uhuru wakuwaza kama tunavyopenda???


@Anony: Haki ya nani sijaokotwa na wala sina hadhi,... kiheshima sihitaji kuheshimiwa kwa kuwa kwani waheshimiwao wanapata nini zaidi ya sie tusio heshimiwaa?

,... na siunajua WATOTO katika kujifunza labda wewe ndio uhribuye kwa kuwa hata jina hutaki tukujue kisa busara zako huna uhakika nazo.

Hivi kwanini hujitaji jina ili tujue MHESHIMIWA ni nani?

Kwa kifupi mie katika kublogu nia sio kuheshimiwa au hata kujipendekeza kwa yoyote na kublogu nimeanza kabla ya wakati ni dili au kuna hadhi za kupoteza:

Ila asante kuwa pamoja na kufikiria niandikacho ni matusi bado unanitembelea. Na nahisi najua wwewe ni nani kama hujastukia ingawa sita kuweka jina hap!:

@Mkuu Gooodman : Mwachie huyu apate therapi ya matatizo yake kwa kunyooshea vidole wengine!:-(:

Anonymous 4:58 am  

nawewe goodman manyanya unamsemea simon unalipwa? au nawewe ni wale wanaopenda kujipendekeza nenda kauze nyanya zako huko sherehe sio yako kanzu inaivalia nini au nawe niwalewale acheni kuunga mkono upuuzi lete hoja zenye kujenga wtz wanamatatizo mengi acheni kupoteza muda kwa mambo ya kipuuzi wakati kuna mambo chungu nzima ya kuwaelimisha wananchi

SIMON KITURURU 7:27 am  

@Anonymous: Nafikiri POINTI yako mara ya kwanza niliipata na usemacho nakielewa na nafikiria hata kabla sijaandika ujinga najua labda niandikacho ni kile ambacho KUBWA ZIMA haliwezi kuandika na kama umesoma posti zangu chini zina lebo Ujinga au UjingaBUSARA. Sasa muache Mkuu Goodmana PHIRI kama vita za kushambulia ujinga unanishambulia mimi na mie nshasema ushanielimisha! na pointi yako nimeipata.


Na najua Tanzania tuna MAtatizo kibao na kama unanisoma zaidi ya posti yangu yenye neno MKUNDU utajua naongelea pia mambo muhimu yahusuyo TANZANIA na pia hata hiyo posti iliyokupandisha jazba ukiisoma tena utajua kuwa lilichokuwa najaribu kuongelea wala sio KINYEO na labda ni uchaguzi wangu wa lugha au maneno ya kuongelea nilichokuwa najaribu kuongelea ndioa mbaya.


Ila naomba matusi au tu chochote HASI wewe mheshimiwa ambaye unataka kutufunza hapa nilenge mimi Simon Kitururu na sio marafikia zangu kama Mkuu Gooodmana ambaye yeye nikiandika ananielewa tofauti kuliko wewe ambaye unabobea kwenye jambo kitofauti!

By the way ASANTE kwa mtazamo wako !
Na kumbuka nia na madhumuni ya blogu au nachoandika hapa wala sio kupandisha jazba mtu! na SAMAHANI kwa kuwa uonacho katika niandikavyo niviitavyo UjingaBUSARA kwako wewe unaona upande wa UJINGA tu na upande wa BUSARA katika ujinga huohuo huoni!


Karibu sana lakini Mkuu na ingekuwa poa sana kama ningekujua angalau JINA ili wakati unanikosoa uwe mwalimu nimjuaye angalau JINA!

Mcharia 11:48 am  

@Simon: Kwanza huyo hajui alisemalo huyo Anonymous....na ndio maana hata jina lake hajui chanzo na lengo kuwepo!!

Hajitambui ndio maana analazimisha mtizamo wake ufuatwe kwa sababu adhanivyo kuwa ni sababu, hajithamini hadi kufikia ya kutumia jina la Anon; sina hakika kama pia anafahamu jinsi kichwa chake kilivyo.

Haelewi kuwa anaouhuru na uwezo wa kuchambua jambo kivyake na kupata ya kufanyia kazi kwa watanzania hao anaodai wanamatatizo KIBAO awaonavyo.

Unajuaje kama wabongo wanamatatizo kiivyo? Tuhakikishie ili tulinganishe na hali ilivyo HomeLand TZ. Lakini pia atupatie na ushuhuda wa kile alichokifanya yeye mara baada ya kuyaona matatizo yalivyo kwa Watanzania.

AU AMESAHAU ALICHOTAKA KUANDIKA HAPA!!??

SIMON KITURURU 12:45 pm  

@ Mkuu Goodman na Rasta Mcharia: Asanteni sana kwa kunielewa na kuweka hilo wazi hadharani!

Mwanasosholojia 4:32 pm  

Wakuu tumsameheni tu huyu anayejiita anonymous, tumetofautiana katika nyanja nyingi, na utashi wa uelewa kwa kile kinachonenwa na mwenzako..labda tu kikubwa ni mtu kuomba msaada wa ushauri makini kwanza inapotokea humuelewi mwingine kabla ya kuanza kumshambulia..lugha ya picha haieleweki na wengi wanaokimbilia kusema ni matusi au kushadadia matumizi ya tafsida...kitu ni kile kile..anonymous siku nyingine nenda zaidi ya appearance...jilazimishe kufika kwenye essence hata kama ni vigumu kwako. Narudia asamehewe asije akasema tunamweka mtu kati bure!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP