Leo katika UCHOKOZI: Si unajua UGALI ni chakula cha KIGENI Tanzania hasa kama ni kweli MAHINDI ni kitu kilicholetwa tu na WAGENI Tanzania?
>> Wednesday, April 27, 2011
Inadaiwa sana kuwa MAHINDI asili yake ni Mesoamerika au tu America ya KUSINI,....
.... kama tu idaiwavyo kuwa ASILI ya MCHELE ni ASIA kitu kiwezacho kuwa wapenda UBWABWA Tanzania ambao wanajivunia vitu vya kiasili Tanzania bado NGUNA ya unga wa MAHINDI na bonge la tonge wakatalo kwenye MISIBA la UBWABWAZ yote ni msaada wa vitu visivyo na asili yake Tanzania!:-(
Swali:
- Ushawahi kuwa unafuatilia asili ya VYAKULA vyako BONGO angalau kujua asili yake ni wapi hata kama hapa tunaongelea MATOKE?
- Hivi WAGENI nishai eeh kwa wenyeji kama kunauwezekano BIA kwa wapenda KILAJI hata kama ni SAFARI ze LAGA wanywacho ni zao la wageni?
Ni uchokozi tu huu wa wazo tu HUU MHESHIMIWA na usikonde!
Hebu Franco akumbushie zao jingine la kigeni MAARUFU Tanzania lijulikanalo kama UKIMWI katika -Attention na SIDA
8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mkuu mimi kila nisomapo, naona chakula(nafaka nk) fulani asili yaki ni nje...mmmh, ina maana sisi kutegemea ni asili yetu...au ndio uchakachuaji wa `hitoria' ili kil kizuri kinatoka nje...nakumbuka hata mayai, makubwa ni ya kizungu, madogo ni ya kienyeji....mh
@Mkuu M3SI unakumbuka historia mara nyingi ni STORI ziegemeazo upande mmoja ....na mara nyingi ni washindi waandikao mpaka ni jinsi gani Sadamu Hussein ndiye aliyekuwa anaua WATU wakati katika hata tafakari za kawaida labda Marekani wauzao historia ya muuuaji Sadam Hussein labda wao ndio wameua raia wasio kuwa na makosa zaidi?
Na tukiingia kwa GADAFI hata siongei ,....
... tukirudi kwenye kipengele cha CHAKULA mtu usipoangalia uanaweza kudhania AFRIKA hakukuwa na chakula hasa jinsi historia ya msosi waichanganyavyo na matatizo ya majanga ya njaa Afrika.:-(
Umeniwazisha upya swala MKUU!
Asante mkuu somo zuri linatufanya tutafakari kwa undani zaidi.
Ninachodhani ni kwamba 'Muwamba ngoma ngozi huvutia kwake'
Christabell
Nakumbuka mwaka wa kwanza kuongea suala hilo kwa upande wangu nilikuwa na baba yangu mzazi kijijini cha Chiduli huko Chilumba, Malawi (29 YEARS AGO) mwaka 1982.
Nusu anitoe roho kwa "kudai uongo kwamba mahindi sio chakula cha asili Afrika".
Ukweli ni kwamba hakuna mwanahistoria popote analolipinga hilo, ila tu, yeye Walter Rodney (katika kitabu chake "HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA"), ndie anaelipinga naye tu kwa misingi ikiwa wabaguzi warangi wanatumia hilo suala kudai 'kwakuwa ukoloni ulileta pia mahindi, basi ukoloni ulikuwa baraka kwa Mswahili'.
Mmmh hapo umenena.
@ Wote:
Nafikiri Christabell anaweza akawa amesawazisha kwa kuwa mengine inabidi tutafiti wenyewe kisayansi ili uwe ni ukweli usiopinginga! Ila
HISTORIA ni kitu cha ajabu kwa kuwa tusipoandika wenyewe tutaandikiwa na matokeo yake ndio haya inafikia mpaka kuna waongeao hawa WAAFRIKA tumewaletea Mahindi tuliyotoa Marekani kusini , Wali tuliowaletea kutoka ASIA, KONDOMu tuwaleteazo kutoka India na ULAYA bado wanakufa kizembe!:-(
Japo kwa mujibu wa Biblia kila zao asili yake ni baada ya uumbaji, lakini bado hata Biblia tuliletewa na hao hao wakoloni enzi zileee...za kutuletea dini na kuchukuwa watumwa.
Na kama ndivyo hivyo; tumekuwa na kawaida ya kuvunjana moyo kuhusu kuandika historia za mambo mbalimbali.
Hivi karibuni nilipokuwa katika mchakato wa kumsaidia baba yangu mzazi kuandika kitabu cha historia ya WAKURYA mtu mmoja alinivunja moyo na kusema...HAKITANUNULIWA.
Nani wa kusoma mahistoria??
Mpaka sasa namshangaa na ninaendelea kumshangaa halafu hatmaye tutakitoa hicho kitabu.
@Mcharia
Samahani kwako na Simon kuchelewa na kommenti yangu hadi leo hii: ikiwa leo (May 8)ni siku ya watu wenye heshima zao duniani: MAMA ZETU KOTEKOTE HONGERA SANA!
Kurudi basi katika topiki yetu ya "uchokozi" wake Simon kama kichwa cha POST yake hapo juu kabisa.
Asili ya chakula haina maana kwamba huyo Hawa na Adam (Waafrika) hawakula chakula hicho zamani za kale, lahasha.
Inamaana tu kwamba (kama moja katika sababu nyingi)kadiri hizo bara zilipotengana (TECTONIC SHIFTS http://en.wikipedia.org/wiki/Plate_tectonics)na kuwa na hali ya hewa tofauti kwa bara zingine, BAADHI YA MIMEA ILIPENDELEA BARA ZINGINE KULIKO ZINGINE.
Sababu za "kuletwa" kwa mahindi hapa na Wazungu (au niseme: "KURUDISHWA KWA MAHINDI NYUMBANI PAKE PENYE BUSTANI YA ADAM, AFRIKA" ni urahisi tu wa vyombo vya kusafiri akina Vasco Da Gama, Mkoloni.
Sisi wenyewe Waafrika ndio wakwanza kutengeneza meli miaka hadi 6000 iliepita na TUKAPELEKA MARA YA KWANZA MAHINDI AMERIKA ILA KUWEZESHA YA KWAMBA WAKATI HALI YAHEWA HAPA KWETU ILIPOANZA KUKATAA MAHINDI, TUWE NAYO AKIBA YETU HUKO AMERIKA!
Vasco Da Gama ni kijana wetu alieturudishia chetu.
Kuhusu yule aliekuvunja moyo kwa kitabu cha Wakurya kwakudai eti hamna mnunuzi naomba nami nikuvunje moyo labda zaidi, yaani niwe AFROPESSIMIST kwa siku ya leo tu.
Unajuwa mtu mweusi, Bw Mcharia, ndio siku hizi tabia yake ya kuwaza malipo kwanza wakati haohao Wazungu waliyetuletea hizo fedha tunawaona kila siku baadhi yao matajiri usiseme.. lakiniwengine maskini wa kupindukia... hujitoa mhanga kusaidia uma bila kuwaza malipo, wengine wanakufa papohapo kwenye VOLUNTEER PROJECTS.
Mpaka leo naamini Mwarabu huyo Bin Laden na mamilioni ya pesa zake alierithi kutoka wazazi wake angekuwa huyo mswahili wa hapa Pretoria au Dar es-Salaam, angekula pesa zake tu bila kujishughulisha na mamabo hatari aliejuwa waziwazi siku moja yanaweza kumtoa roho kikatili!
Imani kwetu Waafrika imeisha; na umebakia unafiki mtupu!
Jana nami nilimpata wa kwangu "mdharau-kitabu-cha-Wakurya". Nilipanda teksi kutoka Jijini Pretoria kwenda Kitongoji cha Atteridgeville na nikapiga gumzo fulani na ndugu mmoja alienifurahisha jinsi alivyokuwa anaelewa siasa, mambo ya kujitoa mhanga, kupigania uhuru na kadhalika.
Lakini nilipomwambia nimeanza blogu kusaidia Waafrika wenzangu kuelewa lugha mbalimbali, kanirukia kwa swali nusu kuangusha teksi aisee:
"UTAPATA MALIPO GANI KWA KAZI HIZO?" akauliza.
Yaani alionyesha kushangaa sana kwamba eti "napoteza" muda na pesa zangu mtandaoni ikiwa hamna alieniahidi pesa!
LAKINI MIMI NDIE NILIEMSHANGAA YEYE ZAIDI. Kwanini aongee uzalendo lakini mawazo yake tele ndani ya pesa tu!!!?
Post a Comment