MTU alichojifunza UTOTONI chaweza kuwa ndio kinalemaza ya UKUBWANI hata yale ya kuhusudu NGURUKA lakini sio DAGAA!:-(
>> Friday, April 29, 2011
Nilichojifunza UTOTONI,...
... haki ya nani chaweza kuwa kinalemaza UKUBWA WANGU!:-(
Na ulichojifunza UTOTONI,...
... kinaweza kuwa ndicho kinacho CHORA RAMANI ya uzungukayo nayo UKUBWANI katika UFANYAYO, upendayo au hata UAMINIYO yale ya ni njia gani unasadiki kirahisi ndio inapeleka watu kwa MUNGU.:-(
Swali:
- AU?
Ndio,...
... labda hata upenzi wako wa UGALI kuliko WALI,....
.... mpaka uchaguzi wako wa MALAYA/changudoa gani utalipia HUDUMA za CHAPUCHAPU kwenye GESTI bubu KAMA IKIBIDI na kama unahisi haitastukiwa na JAMII ijajio WANUNUZI wa HUDUMA za CHAKULA CHA USIKU kwa kuwa wewe ni MHESHIMIWA,...... vyote ni matunda ya ulivyojifunza tokea UTOTONI!:-(
Ni wazo tu hili MKUU!
Ijumaa na WIKIENDI njema!
PS:
Niko Norrköping -SWEDEN kwa muda NAHANGAIKIA tu MAISHA kwa hiyo kama uko mitaa hii tuwasiliane!
Katika kubadili wazo :
Hebu Offside Trick wakiwa na AT warudie-Mduara uko Uwanjani
Au tu OffSide Trick Ft AT wanun'gunike pia ya kuhusu aliwavyo - Samaki
Ngojea tu Offside Trick amalizie tu kwa - Cheza
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
mayo mukulu
Lakini nikikumbuka ya utotoni, sikuwahi kujifunza kuoa, maana hata hivyo tuliambiwa kuna yahusuyo tabia mbaya na nzuri na tukaelekezwa mazuri tu.
Sasa hili la leo la kuwa malaya a.k.a changudoa sijui kama nalo lilifundishwa tangia udogoni..nawaza kwa hapo.
Ninachokumbuka kingine ni kwamba: nilijifunza kupika na sasa imekuwa msaada. Naona si kila alichojifunza mtu udogoni kimekuwa na matokeo kimuendelezo ukubwani.
Sijui, labda kwa wengine ni hivyo.
Unachojifunza utotoni kuhusu kuoa inaweza tu kuwa nikwa kuwaona wazazi wako wameoana kitu kilipalo swala kuoa umuhimu kwako ukubwani.Kuna mambo unajifunza na kufundishwa bila kujijua utotoni
Kweli mkuu, unaweza ukalemaa na utoto, ukubwani ukashangawa. Kuna jamaa alisema hata ukitaka kuchagua kiongozi mzuri angalieni utoto wake alikuwaje, sio lazima, ila kama alikuwa dokozi basi hata akiwa mkubwa atakuwa fisadi...mkuu tupo
Yapo tunayofunzwa na kujifunza,kufunzwa ni kuambiwa Rachel fagio linashikwa hivi,tujifunzayo ni yale matendo tuyaonayo kwa macho,pia hata kwenye michezo yetu ya utoto tunaiga,kama wanawake na kutengeneza watoto na kupika,wanaume na kutengeneza magali na kujifanya wanatoka kazini na.....
Nikweli baadhi ya hayo yanaendelea mpaka ukubwani.
Asante kaka Kitururu na wazo hili zuri la kujifunza/kufunzana.
Nimewaza kidogo.
Ni Ukweli mtupu Simon. Utoto unajenga tabia na muelekeo wa maisha yako. Unachojifunza utotoni, ni mara nyingi sio kwa kufundishwa bali yale uyaonayo na yakubaliwayo na jamii.....utayachuwa kama ni hali ya kawaida katika mtazamo wako wa maisha. Hi ni pamoja na kuchukua changudoas na ubadhilifu wa mali ya umma,,,,uongo nk.
Post a Comment