Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa MAISHANI kuna ASIKIAYE atakacho kusikia, AONAYE atakacho KUONA na atafsiriye ATAKAVYO kutafsiri,.....

>> Friday, April 01, 2011

..... labda  hata WASUKUMA wabisheje kuwa  WALI  sio chakula kama  ilivyo UGALI,...
.... kuna watakao amini UBWABWA sio chakula cha ndege na ni bonge la MGIDO kichakula kama NGUNA tu,...


..... na HAKI YA NANI hata UBISHE ,...
....kuna  atakaye ona NYONYO  wakati wengine wameng'ang'ania kuangalia matako,...
 .... kama ilivyokuwa LABDA kuna atakaye tafsiri salamu zako na uongeayo ni MATUSI wakati  wewe unafikiri unatongoza kwa nidhamu  TU na ustaarabu.:-(

Swali:
  • Kwani si unakumbuka wakati unaangalia  au unasikia kitu na watu wengine-  uwazavyo akilini wakati huo na wawazavyo wengine waangaliao kidude hichohicho  na wewe WAKATI HUO MMOJA-  mnaweza kuwa mnatofautiana MUWAZAVYO ndio maana  MALAYA yuleyule udhaniaye ananuka naye bado ana wateja?

  • Si unakumbuka  stori hiyohiyo moja YA kutia watu MOTISHA na yenye madhumuni ya kupandisha watu MORI  kijazba ile IKUKASIRISHAYO -  inaweza kufanya watu wengine WACHEKE kwa kudhania STORI HIYOHIYO inachekesha na ndio maana PILIPILI ikuwashayo kunawadhaniao ni TAMU?

  • SI  pia UNAKUMBUKA maishani  kuna wastukiao BUSARA katika yale wewe udhaniayo ni UJINGA?


Ndio,...
.... kwa kuwa MAISHANI  kuna ASIKIAYE atakacho KUSIKIA,...
....AONAYE atakacho KUONA,...
... na ATAFSIRIYE atakacho KUTAFSIRI,...
.... lakini bado  MTU akitaka KUELEWESHWA wengine waelewavyo ,...
....na KUELEWA wengine labda inawezekana pia!:-(

Swali:
  • Si inasemekana maishani kuna mpaka wapotezwao na WENGINE?
Ndio,...
... labda tukumbuke tu kuwa,...
.... kabla ya kufikia HITIMISHO kuwa wakati tunaangalia KITU  mitazamo yetu  ndio jinsi KARIBU watu wote ya KITU  kitazamwavyo,...
..... tukumbuke tu kuna wafikiriao chupi wakati wanatazama KITU  na si kila aliyefumbua MACHO na kuyaelekezea kwenye KITU ni kweli anaangalia KITU hasa ukizingatia  labda ni YALE TULIYO YAELEKEZEA FIKIRA ZETU na wala sio MACHO ,...
.....ndio labda TUYAONAYO, tuyasikiayo na TUYATAFSIRIYO.:-(

Ni wazo tu hili MKUU!:-(
Ijumaa naWIKIENDI njema MHESHIMIWA!


Hebu Barrington Levy abadili kwa kuanzisha upya kwa-She's mine
Barrington Levy aendeleze kwa - Shine eye girl

Adinye pia -Black Roses/Here I ComeSijui kwanini -ila ghafla hebu tu D'Angelo abadili tena kwa kurudia -Brown Sugar


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:17 pm  

Ndivyo ilika katika ulimwengu huu. nimepita tu kusalimia na kupoteza mawazo kidogo bado sijatengamaa...

emu-three 2:21 pm  

Ndio kwa ufupi maisha ni demokrasia ya nafsi...TUPO MKUU, ANGALAU KUPITISHA MACHO MAANA WENYE NACHO HAWATUPI NAFASI!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 3:33 pm  

Ni maluweluwe tupu! Hakuna uhalisia!

SIMON KITURURU 2:45 pm  

@Yasinta: karibu sana Mtoto mzuri!
@M3:Tuko Pamoja!
@Mkuu MMN:

Sina uhakika kama nimekuelewa!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP