Kwa MBWA ambaye hajaona MBWA KILEMA anaweza kuapa yahitajika miguu MINNE ili KUTEMBEA,...
>> Wednesday, September 07, 2011
.... wakati KUKU katika ushahidi wake kwa KUKU wenzake ,...
.... anaweza KUAPA ni MIGUU miwili tu yatosha kutembelea hata kwa maringo ,...
..... kwa kuwa tokea anatotolewa ndicho ashuhudiacho hata kwa Machekibobu na Vishtobe vya KIKUKU hata wakati wa kufukuzana ili kufanikisha maswala ya uroda- miguu miwili tu inatosha kutokea baruti!:-(Swali:
- SI yasemekana azoeaye GARI kabla hajaona PIKIPIKI au baiskeli anaweza kuapa yahitajika MATAIRI MANNE au zaidi ili kitu KUTEMBEA huku kimetulia BARABARANI kiusafiri?
Ndio,...
........ labda MENGI yanawezekana kuliko tufikiriavyo,....
..... ndio maana NYOKA hana MIGUU na bado safari hata za kuwinda mademu ya KINYOKA kama tu za kufukuzia maakuli ya aina ya PANYA anaweza bila MIGUU hata isiyo na matege kama limpenzi lako.:-(Swali zaidi kiduchu:
- SI unajua kukwama kwako katika kitu kama GIZA labda wala sio kikwamishavyo WATU wengine katika KITU kwa kuwa kwao hao WENGINE- kwao ni kawaida hata kutembea gizani wakati JICHO ni kupapasa njia na pua ni kielelezo cha upande gani kuna choo?
- SI kwa aonaye yasemekana anaweza kusahau kuwa kutomasatomasa kwatosha hata katika swala la KUJUA ni NDIZI gani zimeiva bila kusahau pia katika KUTATUA lile tatuzi la kifua gani ni cha toto JIKE lililovunja ungo tayari?
Ndio,....
..... yasemekana mazoea NDIO yageuzayo kitu kuwa kawaida,....
.........na yanaweza kusababisha visivyokawaida kudhaniwa havitatui swala,...
..... kitu kiwezacho kufanya MBWA aamini ili kutembea inahitajika MIGUU minne,....
.... wakati BATA anajua kuwa MIGUU miwili inatosha katika kutembea kwa kuwa katika maisha yake kashafikia kukubuhu MPAKA kwa kutembea tena huku anaharisha- na HILO kwake ni kawaida kama MIDUME kukojoa imesimama.:-(Swali:
- AU?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA ,...
.... na nakutakia kila kheri katika kustukia labda KIKUKWAMISHACHO sio kwamizi kihivyo,...
.... bali ni kwa kuwa tu kivyako unaona KIVYAKO wakati kwa mwingine bado wewe HUJAKWAMA kwa kuwa kwa WEWE kufikiria unahitaji angalau MAWILI - mwingine bado anaona kwa MOJA ULILONALO yawezekana.:-(
NIMEACHA!:-(
Hebu katika kubadili wazo Jeromarsh alete swala la ki-YESUYESU tena katika -Twede
Youssou N'Dour amrudishe-ALLAH
Kabla BUJU BANTON hajaingilia kati na kurudisha tu -AFRICAN PRIDE
8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Bata,na mbwa ,nimependa mifano yao.Vilevile yawezekana,miguu miwili ya bata,ikamshangaza bata huyo na kumtofautisha, kwa kuona miguu minneya mbwa ikimsaidia mbwa kuogelea, pamoja nasifa aliyo nayo bata ya kunya hovyo lazima azime fegi!!?
tuko pamoja mtakatifu.
Kaka S.
Duh! Mtakatifu na wewe kaka Sam mbona mna mifano ya mafumbo sana? hakika sijui nisema nimecheka au nimelia?:-)..:-(
Halafu sijui ni mgongano gani wiki hii nimekuwa nikimsikiliza huyo kijana Jeromarsh----
@Kaka S: Ndio hapoo!
@Da Yasinta:Mmmmh!
Da Yasinta,na ushangae ,mazoea yalivyo kuwa mabaya,mtu/mwanamke anapigwa na mumewe nahii siyo kijijini tu hatamijini,ukimuuliza vipi mbona jicho limevimba atakuambia/kukujibu nimeanguka!! kumbe kadundwa.mazoea hayohayo kwa ko wewe da,Yasinta utashangaa kwanini mtu ampige mkewe.na ndiyo maana dume likipigwa namkewe ina kuwa sooo!!!,kwani nimazoea kuona ni mwanamke anapigwa.mfano usikie kitururu(mtakatifu) kapigwa namkewe au mimi sam (kaka s)nimedundwa na mkewangu,pata picha tunalala mika kwa kipigo!!? anyway ,kaka s
Mhhhh kakas na Kitururu nimewavulia kofia!!!!mazoea yanatabu auu.
Rachel! afadhali umekuja kunisaidia hapa...mweh? Kwa hiyo hapa Kaka S. unataka kusema kuwa wanaume ni wavumlivu na wanawake walalamikaji...Haya...
@Da Rachel: Kweli kabisa kama alivyosema Kaka S, Mazoea yanatabu zake! Unaweza mpaka ukaamini kila krismasi unahitaji nguo mpya ambayo sio chupi ati!:-(
"..... ndio maana NYOKA hana MIGUU na bado safari hata za kuwinda mademu ya KINYOKA kama tu za kufukuzia maakuli ya aina ya PANYA anaweza bila MIGUU hata isiyo na matege kama limpenzi lako.:-( ...."
Mama mmoja tena mzima kabisa, rafiki yangu A.Kusini aliniambia siri yake hivi: "nikitaka shibe kabisa namtafuta kilema! Tena mume wangu hana wasiwasi kwakuwa anawadharau ndugu zetu hao vilema"
:-(
Post a Comment