Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati NIMECHACHA na sina hata PESA za kulipia kikojolewa ,.. SAMAHANI labda KUMBUKA sina msosi NYUMBANI,......

>> Saturday, September 10, 2011

.....lakini naomba nikopeshwe ANGALAU nikachangie harusi ya JIRANI nisije nikaaibika,...
....kwa kuwa kuna uwezekano  NITAAIBIKA  ndani yangu KIMIMI tayari  kisa NIMEOMBA ,...
..... kwa kuwa kitiacho aibu kitafsiri zangu LABDA kishaathiriwa na TAFSIRI ZA JAMII ,...
... na tayari KIMIMI,...
....... na mie katika KICHENI PATI YAKO  ambayo unachekelea sana michango ambayo moja ya mchango ni labda ni WANGU ,...
 ..... labda kumbuka kuwa  watoto wangu LABDA  hata KIMAMA KISEBENGO LABDA wamelala na njaa  ili uniheshimu  kimichango nisiyoiweza  MWENZIO ila kwakuwa ni jirani yako inabidi nichangie ili nisije onekana na ROHO mbaya MTAANI!:-(

Swali:
  • Si umestukia LABDA kuna ambao hawastukii kuwa wengine yao kwetu GHALI ndio maana LABDA malaya zetu wabaya KULIKO MALAYA ZAO ingawa twapenda kununua malaya WAZURI KAMA WAO  kwa kufikiria LABDA  angalau angalau hata kimalaya zetu kama tu kimalaya zao labda bado   ukinunua BADO AHADI NI ZILEZILE  kuwa hubabaishwi katika ahadi za kugewa?
Ndio,...
.... yasemekana usipotembelea MISIBA ya WENZIO,...
.... na hao wenzio watakususia MSIBA,...
... kitu kifanyacho kuna  wenye madeni kuliko mtaji wa kujenga NYUMBA kisa michango ya HARUSI na KICHENI pati za watu!:-(

Swali:
  • Hivi katika jitihada za MTU kuonekana MTU MZURI hata kwa asiyoyaweza- UTU UZURI sio aina ya UTUMWA?

Ndio,...
.... katika jitihada za KUONEKANA ni WATU WAZURI,...
... kuna MIMTU  yasemekana imeshageuka MITUMWA!:-(



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu tu tena STEEL PULSE waingilie tena shughuli kwa-RALLY ROUND






Steel Pulse warudishe tena - Sound System



Steel Pulse warudie tena- Chant A Psalm




Kabla tu Aswad hawajaingilia kati kwa- Give a little love



Au ngojea tu Aswad waongezee dozi kwa- Need Your Love



JUMAMOSI NJEMA MKUU!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 1:22 am  

Utumwa huu wa kuonekana umechanga wakati,watoto wako hawana uhakika wa kwenda chooni,una kosti watu wengisana,hasa sisi wabongo. tatizo kubwa ni kutokuwa wa kweli kwa nafsi zetu,na pia kwa jamii inayo tuzunguka.sifa inatuponza sana,zamani nilikuwa hivyo niliona niaibu mtu akiniomba mchango halafu nisitoe,pia wakati mwingine hata huombwi mwenyewe unajishitukia,na hii ndo mbaya zaidi.unajishitukia kuwa badala ya kutoa elf 30ambayo kwakweli ndiyo ubavu wako,badalayake unasema lakimoja kwa mbwembwe nyingi,lakini mwisho wake,unashindwa kutoa.hapo unakuwa si utumwa tu bali hata kutoaminika,muongo,hatakutengwa waweza tengwa.unabaki unajisikia vibaya,unashindwa hata kwenda kusema jamani niliahidi lakini mambo siyo mazuri,watu watakuelewa.mtakatifu kunakazi sana heri yako wewe.kaka S.

Simon Kitururu 11:44 am  

@Kaka S: Yani umemaliza Mkuu wala hata sina nyongeza baada ya kukusoma katika hili!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP