Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika swala la: ``KATIKA ajali hii wamefariki WATU KUMI na WAMASAI wawili!:-(´´

>> Friday, September 09, 2011

Duniani inasemekana kuna mpaka maswala ya;....

....Akifa MYAHUDI MMOJA na akifa MPALESTINA MMOJA kuna tofauti,......
......kama tu ukifanananisha  tofauti za  AKIFA MMAREKANI MMOJA wakati WATANZANIA KUMI na ISHIRINI  elfu wanakata roho ni nani vyombo vya habari vita wasononokea,...
.... kitu ambacho kinatisha hasa kwa kuwa inaaminika BINADAMU wote ni SAWA eti!:-(

Swali:
  • Umestukia hata katika  maswala ya 9/11 ambayo yanaliza WAMAREKANI sana  ukihesabu idadi ya MAREHEMU halafu ukaenda kuhesabu ni WAIRAKI wangapi WAMEFARIKI chini ya WAMAREKANI unaweza kupata kizunguzungu  kwa kustuka kuwa LABDA BINADAMU si sawa?
  • Kwani hujastukia kuwa  ISRAELI akifa  MYAHUDI mmoja   malalamiko yake labda ni sawa na pale wakifa WAPALESTINA  elfu moja?
  • SI unakumbuka pia kuwa zaidi ya WAKONGO milioni kumi walifariki chini ya MFALME wa KIBELGIJI kitu ambacho husikii  wakati  kila mtu  hukumbushwa ni jinsi gani HITLER mbaya kwa  yaliyowatokea WAYAHUDI?


Ndio,...
.... yasemekana TANZANIA hata ukiandamana  unaweza ukabwengwa virungu au kupigwa risasi na MGAMBO wa Ki-F.F.U  ambaye ni jirani yako  umfundishiaye WANAE kinyama kuliko  ukidakwa UNORWAY wakati unaua HALAIKI ya watoto kama alivyofanya Anders Behring Breivik,....
...... ambaye kivyao bado wanamhukumu KIUTU muuaji asiyeonyesha UTU kwakuwa wanadai wanatoka katika jamii ijaliyo UTU!


SWALIZ  zaidi kiduchu:
  • SI inasemekana WAAFRIKA kwa ujumla hatujali UTU ndio maana siye wenyewe kwa wenyewe hatujali WATU na maisha yao?
  • SI nasikia kunawadaio ukileta MBWA anyanyaswaye wa MMAREKANI na kumuweka katika gereza la Tanzania na kumfunga wafungwavyo WAFUNGWA BINADAMU wa KITANZANIA na WATANZANIA wenzao KISEREKALI kuna wasiobisha labda MBWA huyo ataingiwa wazo la KUJINYONGA hata kwa kamba za migomba?


Ndio,...
..... hata tukiachana na WAMAREKANI , Wayahudi,....
....nk.... na kujichungulia siye wenyewe wa BONGO NYOSO,...
..... labda kuna uwezekano siye WATANZANIA hatujali uhai kama wajalivyo wengine ,...
... na ushahidi unaweza kuwa hata ule mdogo tu wa jinsi tusivyoshangaa AJALI za BARABARANI ziuavyo utafikiri ni kitu cha kawaida,...
.... hata kabla hatujachungulia ule mfano wa ni nani anatishwa sana na KIBONGE mzuri kama malaika hata kama tunasikia ana UKIMWI kumuingilia maungoni PEKUPEKU kisa hatuna uhakika atakuja kukubali tena kesho baada ya pombe kumtoka KICHWANI!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu turudi BONGO ili THE KILIMANJARO waanzishe mashambulizi kwa -KINYAUNYAU




Mombasa Roots wadindishe kwa - Disco Chakacha




Safari sounds band waongezee dozi tena kwa -Mama lea mtoto wangu




THE KILIMANJARO wajibu mashambulizi kwa-KINYAMA NYAMA HICHO/Boko




MOMBASA ROOTS waingilie shughuli tena kwa mdinyo-KATA




Au hebu turudi KONGO ili Papa Wemba alainishe tu kwa - Shaana


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP