Kwa MBAYA WAKO apendaye chupi ,... huwezi KUSHINDA hata kwa chupi nzuri ile SAFI!!
>> Friday, September 09, 2011
Kwa MBAYA wako,...
...... chochote ufanyacho kizuri ,...
..... kwa bahati mbaya YASEMEKANA atafanikiwa tu kukitafutia KASORO mbaya!:-(
Swali:
- Lakini si unajua MBAYA wako akupondaye KWA MAZURI UFANYAYO yasemekana kiundani huwa anafahamu afanyacho ni kukufanyia UBAYA tu?
Ndio,...
.... labda pia kumbuka katika YAKO kuwa ,...
..... kuna uwezekano kuna WAHUSUDUO MTU wafumbiao tu MABAYA yake ,...
.... hata kama wanajua afanyayo ni MABAYA!:-(Tunakumbushana tu MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA!
Hebu tugeweshule ya maswala ya kimazingira ghafla katika-300 Years of FOSSIL FUELS in 300 Seconds
Au tu ALPHA BLONDY aingilie kati kwa - I Wish You Were Here
Alpha Blondy aongezee dozi ya utamu kwa kidude- Travailler C'est Trop Dur
Kabla tu Immortal Technique hawajaingilia nakubadili kidogo mshwawasha kwa - Creation &Destruction
Halafu tu Israel Vibration warudishe kidude palepale tu kwa -Feelin' Irie
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ijumaa njema nawe pia Kaka Simon...Nimeupenda wimbo huo wa kwanza "Alpha Blondy - I Wish You Were Here "
Nimependa, mfano wa mpenda chupi,chupi na hata gagulo pia ni moja ya vitu muhimu kwa dada zetu,hasa wabongo,sijuwi kama mpaka sasa gagulo linavaliwa. haya mbaya wako niaduwi yako kama ilivyo rushwa,kuitwa adui wa haki,pia hivyo hivyo kwa mbaya wako.kama alivyo sema Simon kizuri chako chaweza kugeuzwa kiba na mbaya wako,mpaka mwenyewe ukashangaa.mfano waweza kuwa umewekele kanyau chupi safi na mpya, na kwakuwa siyo rahisi kwa mtu mzima kuonyesha chupi hadharani kwa mila zetu,basi hapohapo mbaya wako atachukua fulsa ya kuku geuzia kibao,kwamba chupi yako imetoboka,na akikwambia uvue uoneshe hakika huwezi,kutokana na mila zetu.utabakia kusema jamani watuwengine sijuwi vipi.lakini kwa njia nyingine usha umbuka.anyway chupi,na gagulo we acha tu. kaka S.
@Yasinta: Alpha Blondy kuna baadhi ya nyimbo zake huwa zinanikosha sana!Ijumaa njema kwako kwa maranyingine Kipenzi!
@Kaka S:Ila inasemekana ni makosa KUUMBUKA kwa KUSINGIZIWA yasiyo kweli lakini,...ila tatizo ni udhaifu wetu WANADAMU hasa siye tutokao katika jamii zisizo``INDIVIDUALISTIC´´ kisana,... kwa kuwa twajali sana yawengine yanatuhusuje kitu kifanyacho hata waliochacha wanajikuta wanachangia KITCHENI PATI za watu kwa kuogopa kujiharibia sifa kwa wengine katika jamii.
Mtakatifu,hebu tuangalie, kampani unayo kunywa nayo pombe, ukiwa ulaya, nakampani unayo kunywa nayo pombe ukiwa tanzania,ni wapi ujisikia raha au unaridhika na mazingira yake ya uwapo katika kundi hilo la washikaji wako,iwe ulaya au bongo?.na ukienda mbalizaidi,katika makundi yote hayo mawili ndani yake ,hukosi wabaya wako/mbayawako.Lazima kuna kitu kwa upande wa bongo ambacho kwa mkusanyiko huo utasemwa kwa mabaya ama kwa mazuri,na ikitokea mfukoni ukatetereka kidogo kwa sababu zilizo ndani ya uwezowako,upande wa pili watahesabu ushindi,kwamba ,mbona hatuoni,makali ya ulaya.naam nakwambia mtakatifu,kwa mazingira hayo ndo maana sisi wabongo tuna kwamishwa na usemi huu, watu watanionaje mimi nisipo wanunulia pombe,nisipo wapamchango wa harusi, hataumeshiba ukisema asante unaogopa watakufikiria vibaya.nahivi ndiyo tulivyo tunaweka jamii yetu mbele wewe baadaye.haya nisiende sana .tuko pamoja. kaka s.
@Kaka S: Katika maswala ya KILAJI nafikiri kuna tabia tofauti kati ya WABONGO na watu wengine kwa kuwa huwa nazikuta tabia za KIBONGO ulaya kama kawaida kwa WABONGO.
Kwa hiyo mitaani huku ughaibuni misengenyo ipo tu katika baadhi ya vikao nivipitiavyo kupata moja , mbili, tatu, nne, tano.... zile Moja baridi moja moto . Ila katika viwanja ambavyo wabongo sio wengi ni fulu kila mtu kivyake na mambo zake kwa hiyo MTU hutishi na wala hutishwi.
Ila BONGO mara kadhaa nishasikia nikitetwa jamaalimefukuzwa ughaibuni kisa wanahisi nimekaa sana BONGO na pia mfano wa kuonwa fala kisa huna cash yameshanikuta na kirahisi unaweza kukimbiwa na wajifanyao MARAFIKI kwa kudhania utawapiga mzinga.:-(
Ila kikubwa mie naona tunapitiliza pale ambapo inafikia tunaogopa JAMII inatufikiriaje mpaka tunajiingiza utumwa ilitu tuonekane wamaana kwenye jamii!.:-(
Post a Comment